Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Mahakama yawaachia huru askari nane waliodaiwa kusafirisha shehena ya dhahabu

67321 Wafungwapic

Thu, 18 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza imewaachia huru askari wanane waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kwa kusafirisha kilo 319 za shehena ya dhahabu na Sh305 milioni.

Uamuzi huo umetolewa leo Alhamisi Julai 18, 2019 na Hakimu Mkazi mfawidhi, Rhoda Ngimilanga baada ya wakili wa Serikali mkuu, Castus Ndamugoba kuieleza mahakama hiyo kuwa ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka nchini (DPP), haina haja ya kuendelea na kesi hiyo.

Uamuzi huo wa Mahakama umefanywa baada ya jana Jumatano, DPP, Biswalo Mganga kutangaza kuifuta kesi namba moja ya mwaka 2019 ya uhujumu uchumi iliyokuwa inawakabili askari hao.

Biswalo alisema kesi hiyo imefutwa kwa sababu ya maslahi ya Taifa.

“Nimeifuta kesi hiyo kwa sababu ya maslahi ya Taifa kwani kuna mambo mengi yanayohusiana na Taifa,” alisema Biswalo

Askari hao ni Mkuu wa Operesheni mkoa wa Mwanza, Morice Okinda, E 6948 D/CPL Kasala, F 1331 PL Matete, G 6885 D/C Alex na G 5080 D/C Maingu.

Habari zinazohusiana na hii

Wengine ni G 7244 D/C Timothy, G 1876 D/C Japhet, H 4060 D/C David Kadama ambao walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Januari 11, 2019.

Askari hao pamoja na wafanyabiashara wanne walikuwa wakikabiliwa na makosa matano ya kutakatisha fedha, uhujumu uchumi na kula njama za kupanga uhalifu, makosa waliyodaiwa kuyatenda kati ya Januari 4 na 5, 2019.

Columnist: mwananchi.co.tz