Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

MWANANCHI JUKWAA LA FIKRA: Bajeti na uwekezaji hafifu unavyotishia ubora wa elimu

75766 Jukwaa+pic

Mon, 16 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tangu Serikali ya awamu ya tano iingie madarakani mwishoni mwa mwaka 2015, kumekuwa na mafanikio katika sekta ya elimu likiwamo ongezeko la wanafunzi wanaoandikishwa katika elimu ya msingi.

Uandikishwaji wa wanafunzi wa shule za msingi umeongezeka kwa asilimia 17 kutoka wanafunzi 8,639, 202 mwaka 2016 hadi wanafunzi 10,111,255 mwaka 2018, huku wanafunzi wa shule za sekondari ukifikia asilimia 12.6 kutoka wanafunzi 1,908,857 mwaka 2017 hadi 2,148,466 mwaka 2018.

Kwa jumla, uandikishwaji wa wanafunzi wa shule za msingi umefikia asilimia 96.9 na asilimia 70 ya wanafunzi wanaomaliza darasa la saba wanaendelea elimu ya sekondari.

Hata wanafunzi wanaoingia elimu ya juu pia wameongezeka kwa asilimia 12 kutoka wanafunz8i 189,732 mwaka 2015/16 hadi wanafunzi 211,558 mwaka 2017/18.

Licha ya ongezeko hilo, changamoto bado imekuwapo kwenye ubora wa elimu ukihusisha uwekezaji mdogo katika elimu. Ongezeko la wanafunzi haliakisi uwekezaji wa fedha katika sekta hiyo ktika miundombinu, walimu na vifaa vya kufundishia.

Wakati kumekuwa na wastani wa ongezeko la asilimia 17 ya wanafunzi, shule shule zilizojengwa ni sawa na asilimia 1 tu za msingi na sekondari.

Pia Soma

Advertisement
Kwa mujibu wa taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2016/17 shule za msingi zina upungufu wa asilimia 85 wa madarasa upungufu wa asilimia 83 vyoo vya shimo, upungufu wa asilimia 66 walimuna upungufu wa asilimia 14 wa madawati.

Kadhalika, shule za sekondari nazo zina upungufu wa madarasa kwa silimia 52, upungufu wa maabadra kwa asilimia 84, madawati kwa asilimia 86, upungufu wa nyumba za walimu kwa asilimia 85, upungufu wa mabweni kwa asilimia 85 na upungufu wa vyoo kwa ailimia 53.

Kulingana na ripoti ya Shirika la Hakielimu ya mwaka 2018, uchambuzi unaonyesha kupungua kwa bajeti ya Wizara ya Elimu kwa kipindi cha miaka minne kutoka Sh 4.77 trilioni mwaka 2016/17 hadi Sh4.7 trilioni mwaka 2017/18 na Sh4.62 trilioni mwaka 2018/19.

Anguko hilo la kibajeti linakuja wakati bajeti ya Serikali imekuwa ikiongezeka kutoka Sh29.54 trilioni hadi Sh31,7 trilioni na Sh32.47 trilioni.

Uwiano kati ya bajeti ya Serikali inayotengwa katika elimu imeshuka kutoka asilimia 17 mwaka 2015/16 hadi asilimia 14 mwaka 2018/19.

“Hali hiyo siyo tu inaonyesha kupungua kwa kipaumbele cha Serikali kwa elimu bali pia inaonyesha kushuka katika viwango vya kimataifa kama azimio la Dakar linalotaka kutengwa kwa angalau asilimia 20 ya bajeti kuu ya Serikali katika sekta ya elimu,” imesema ripoti ya HakiElimu.

Mbali na bajeti, Serikali pia imekuwa ikitenga fedha za ruzuku kwa ajili ya kuhudumia wanafunzi. Lengo la fedha hizo ni pamoja na ukarabati wa Vifaa asilimia 20, vitabu vya kiada, Viongozi vya walimu, vifaa vya ziada vya kusomea asilimia 40, chaki, madaftari, kalamu za risasi na za wino asilimia 20, gharama za utawala asilimia 10 na karatasi za mitihani manunuzi na kuchapisha asilimia 10.

Maoni ya wadau wa elimu

Ofisa wa Shirika la Twaweza, Teli Godfrey anachambua uchangiaji wa elimu kwa Serikali na wananchi akisema Sera ya Elimu iliyoanzisha elimu bila malipo umepunguza ari ya wananchi kuchangia huduma hiyo.

“Pamoja na Serikali kutoa elimu msingi bila malipo, bado uchangiaji wa wazazi ni wa muhimu. Kwa muda sasa mwamko wa wazazi kuchangia umeshuka, kwa sababu kwanza walizuiwa baada ya Serikali kutangaza kutoea elimu bure ilileta mkanganyiko,” anasema Godfrey.

Mbali na wazazi kutochangia, anasema hata bajeti ya maendeleo na ruzuku inayopelekwa katika sekta ya elimu haifiki kwenye maeneo yanayokusudiwa kuboresha elimu.

“Wanalenga kwa mfano kuongeza idadi ya wanafunzi au kuongeza miundombinu pekee, lakini hawaangalii ubora wa elimu,” anasema na kuongeza;

“Kuna mambo ya muhimu kwa wanafunzi ili kuimarisha ubora wa elimu kama chakula kwa wanafunzi, mazingira mazuri ya kujifunzia, kama maji safi, vyoo na walimu wa kutosha.”

Anasema baadhi ya wanasiasa wanaichukulia elimu kama kete ya kujipatia umaarufu.

“Mara nyingi wanasiasa wanapeleka maendeleo yanayoonekana tu, ili hatimaye aje kusema ametekeleza ilani au ahadi, bila kujali hayo maendeleo yanachangia kwa kiasi gani ubora wa elimu.”

Hata hivyo, anapongeza uwahishwaji wa ruzuku za elimu tofauti na awamu iliyopita.

Akizungumzia mahitaji ya elimu, Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Leah Ulaya anasema wamekuwa wakiishauri Serikali kuongeza bajeti hasa upande wa masilahi ya walimu.

“Tumekuwa tukishauri Serikali kuongeza masilahi ya walimu ambao ndiyo wafundishaji. Tunashukuru kwa sasa walimu wanapandishwa madaraja, lakini bado tunaendelea na mazungumzo na Serikali,” anasema.

Kuhusu uchangiaji wa elimu, Ulaya anasema kwa hali ilivyo kwa sasa kuna haja ya wazazi kuendelea kuchangia ujenzi wa miundombinu na huduma nyinginezo, kwa sababu mchango wa Serikali pekee hautoshi kugharamia elimu.

Columnist: mwananchi.co.tz