Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

MAKALA YA MALOTO: Dk Bashiru anateswa na Katiba ya CCM

76363 Bashiru+pic

Thu, 19 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tamko la Katibu Mkuu CCM, Dk Bashiru Ally hivi karibuni akuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na wa Mbeya, Albert Chalamila watakuwa wa kwanza kurudishwa darasani kusoma uongozi, inaakisi maumivu yake ndani kwa ndani.

Dhahiri ni kwamba, Dk Bashiru anawaona Makonda na Chalamila si viongozi wanaotosha na kwa vile hana kitu cha kuwafanya, amekuwa akilalamika. Mwisho ametangaza kuwarudisha darasani kusoma uongozi ili wawe viongozi wazuri.

Tamko la kuwarejesha darasani wasome uongozi, linabeba maudhui kuwa hawajawa viongozi wazuri. Tafsiri ya kiongozi ambaye si mzuri, huyo ni mbaya. Kwa maana hiyo, katika tathmini ya Dk Bashiru, Chalamila na Makonda ni viongozi wabaya. Na ukisema mtu ni kiongozi mbaya, unamaanisha hafai kuwa kiongozi.

Kwa mantiki hiyo, ni rahisi ‘kubeti’ kuwa Dk Bashiru angekuwa na mamlaka ya kuamua nani awe kiongozi na yupi asiwe, Makonda na Chalamila wasingepenya. Kwa vile mwenye mamlaka ni mwingine na yeye hana la kupinga, amechagua kulalamika. Hana namna nyingine ya kufanya.

Hutakosea pia ukisema kwamba matamko ya Dk Bashiru yanalenga kumpa ujumbe mwenye mamlaka awaondoe wahusika kwenye nafasi zao.

Maneno “rudi shule” ni msemo wa kawaida, unaomaanisha kuwa anayepewa ujumbe hajafuzu eneo analohusishwa nalo. Ukimwambia daktari arudi shule, ni ujumbe kwamba hajawa na daktari mzuri, hajafaa udaktari.

Pia Soma

Advertisement
Bashiru ndiye katibu kkuu wa chama kinachoongoza Serikali. Ni mwenyekiti wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM. Cheo hicho kinampa hadhi ya kuwa mtendaji mkuu wa chama.

Serikali iliyopo madarakani ipo kwa sababu ya CCM, na Dk Bashiru ndiye injini ya CCM kwa sasa. Pamoja na hivyo, hana uwezo wa kufanya chochote ndani ya Serikali.

Mamlaka ya Bashiru kama Katibu Mkuu CCM, yapo ndani ya majukumu ya Sekretarieti ya CCM ambayo yamegawanywa katika makundi mawili. Mosi, Kusimamia shughuli zote za utendaji za chama kitaifa. Pili, Kuandaa shughuli za vikao vya chama ngazi ya Taifa. Yeyeni moyo wa CCM, chama kinachounda Serikali, lakini hana mamlaka yoyote ndani ya Serikali, inatakiwa apaze sauti, Rais amsikie, ikimpendeza aamue.

Ni kwa sababu majukumu ya Bashiru kama kiongozi mkuu wa sekretarieti ni kusimamia shughuli za utendaji wa chama na kuratibu vikao, ni msimamizi wa wakuu wa idara za chama, yaani makatibu wa halmashauri kuu. Hao ndio anaweza kuwa na sauti ya moja kwa moja.

Kumbe sasa, kinachomtesa Bashiru ni Katiba ya CCM, haijampa mamlaka yoyote ndani ya Serikali. Miaka ya nyuma, Katiba ya CCM ilikuwa inatoa mwanya kwa sekretarieti kumwita mtendaji yeyote wa Serikali inayoundwa na chama hicho, kisha kumwajibisha, isipokuwa Rais ambaye anakuwa mwenyekiti wa chama.

Sasa basi, kipengele hicho kingekuwapo kwenye katiba ya sasa, maana yake Bashiru asingekuwa analalamika kuhusu Makonda na Chalamila kuwa wanahitaji kusoma uongozi, bali angewaita kwenye sekretarieti na kuwashughulikia.

Hivi karibuni Chalamila alitoa kauli nzito, aliruhusu wezi na vibaka kuuawa wakikamatwa. Chalamila pia akaagiza waliokamatwa kwa tuhuma za kumrushia mawe mmoja wa wakuu wa wilaya Mbeya, wapigwe na hata wafe kwa sababu wao walidhamiria kumuua mkuu wa wilaya.

Hizo si kauli za uongozi. Inasikitisha kwamba Chalamila alizitoa baada ya kuwa ameshakosolewa na Bashiru na kutangaza kumrudisha shule. Ni dhahiri kuwa Chalamila hamhofii Bashiru, ndio maana haonyeshi kujirekebisha.

Chalamila angejua kuna eneo Bashiru anaweza kumshughulikia, angeshajirekebisha. Kuna mabadiliko yangeonekana. Kama matamshi ya Bashiru, yangepitia kwa Mwenyekiti wa CCM, Dk John Magufuli, Chalamila asingenadi mauaji. Angekuwa na angalizo. Maana kwenda kinyume na Rais Magufuli, maana yake ni kuweka rehani cheo chake.

Unaweza vipi kurudia kutoa matamko ambayo yalimfanya kiongozi wako aseme hufai? Unadhani Dk Bashiru anajisikiaje kuona Chalamila na Makonda hawajirekebishi licha ya kuwaonya?

Columnist: mwananchi.co.tz