Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

LIVE: MWANANCHI JUKWAA LA FIKRA

Fri, 24 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es salaam. Wizara ya Kilimo nchini imeanza kufanya mapitio ya Sera ya Kilimo ya Mwaka 2013 lengo likiwa ni iendane na mabadiliko mbalimbali yaliyojitokeza katika sekta hiyo.

Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara hiyo, Obey Assery amesema hayo leo Alhamisi Mei 23, 2019 wakati akizungumza na Mwananchi  kabla ya kuanza kwa mjadala wa Jukwaa la Fikra kuhusu kilimo lililoandaliwa na kampuni ya Mwananchi Communications Ltd (MCL).

Mjadala huo unafanyika leo katika ukumbi wa Kisenga, Kijitonyama jijini Dar es Salaam na kurushwa moja kwa moja na kituo cha Televisheni cha ITV na Redio One.

Assery amesema hatua hiyo inachagizwa na mabadiliko ya teknolojia katika sekta ya  kilimo, mazingira ya biashara na masoko pamoja na ukuaji wa miji.

“Kwa sasa tupo katika hatua ya awali, wiki ijayo tutaanza vikao na wadau wa kanda, tunategemea watajitokeza kwa wingi kwa ajili ya kupokea maoni yao, "amesema Ossery.

Mara ya kwanza jukwaa hilo lilifanyika Juni 28, 2018 likiwa na mada ya Afya Yetu, Mtaji wetu.

Pia Soma

Mara ya pili lilifanyika Oktoba 4, 2019 na kujadili fursa na changamoto kuelekea uchumi wa viwanda.

Mara ya tatu lilifanyika Februari 7, 2019 huku mada ikiwa ni mkaa, uchumi na mazingira yetu.

Columnist: mwananchi.co.tz