Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Kama hatuna ligi bora tusitarajie makubwa

33198 Allan+Goshashy.png Mwananchi Photo

Mon, 24 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Ligi iliyo bora huwezesha kupata wachezaji bora watakaounda timu bora ya Taifa itakayoweza kufanya vizuri kimataifa na pia kupata klabu zitakazotuwakilisha vyema katika mashindano ya kimataifa kwa ngazi ya klabu.

Kama tutakuwa na ligi bora itakayotuwezesha kuwa na timu bora ya Taifa na klabu bora zitakazotuwakilisha vyema kimataifa, basi mafanikio hayo yataweza kukuza na kuendeleza kiwango cha soka katika nchi yetu.

Ninaamini kabisa, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wanafahamu na wanaamini kuwa soka ni mchezo wenye nguvu, unaopendwa na watu wengi duniani na unaoweza kuvutia wengi.

Na ndiyo maana TFF huweka kanuni na sheria katika Ligi Kuu kwa ajili ya kuufanya mchezo wa soka uwe na ladha katika kuucheza na pia uwe na ladha katika kuuangalia na hivyo kuufanya uwe na burudani zaidi.

Sasa tatizo tulilonalo katika Ligi Kuu yetu ni kuhakikisha kanuni, taratibu na sheria za soka zinafuatwa na kuheshimiwa na pia kanuni za uchezaji wa kiungwana zinazingatiwa na wachezaji, makocha, waamuzi, viongozi, mashabiki, n.k.

Ndiyo, nafahamu TFF wamekuwa wakiziagiza klabu, makocha, wachezaji na waamuzi kuzisoma kwa makini kanuni za ligi na kuhakikisha zinaeleweka na kufuatwa kwa faida ya mchezo wa soka nchini, lakini sidhani kama wahusika wamekuwa wakilichukulia suala hili kwa uzito mkubwa na hapa ndiyo tatizo la chanzo cha kukosa ligi bora nchini linapoanzia.

Ni wazi kuwa klabu, makocha, wachezaji, waamuzi na mashabiki wanatakiwa kuelewa soka kama ilivyo michezo mingine yote inalindwa na sheria pamoja na Kanuni. Bila sheria na kanuni mchezo wa soka utakuwa ni vurugu tupu, pia utakuwa hauna heshima, uadilifu, adhabu hazitatolewa na mshindi hatapatikana uwanjani kihalali bali kwa kutumia njia chafu zisizokubalika.



Columnist: mwananchi.co.tz