Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

KUTOKA LONDON : Baadhi ya mazuri niliyojifunza uzunguni

Mon, 26 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kati ya makubwa yanayotupeleka Waafrika Uzunguni ni haki za kufanya utakalo, yaani uhuru Binafsi.

Uhuru wa kujiendeleza kiakili, kihisia, kijinsia na kiroho. Wengi tuna fikra kuwa wenzetu hawaabudu Mungu lakini si kweli. Makanisa na majumba tele ya ibada vimejazana Ughaibuni. Ukweli makanisa hutoa huduma mbalimbali ikiwemo kusaidia wasiojiweza.

Sasa basi ndani ya haki hizi za kujiendeleza huwemo utendaji kazi, kujielemisha na ujasiriamali. Ndiyo maana uvumbuzi na uchunguzi wa kisayansi na kisanaa, huchangamkiwa na kila mtu. Kutoka vifaa vya kiteknolojia hadi bidhaa lukuki tunazotumia duniani.

Ndani ya utundu huu wa kugundua, haki za walemavu ni jambo lililonivutia sana Majuu. Serikali ya Leba, Uingereza miaka kumi na tano iliyopita mathalan, ilikuwa na Waziri kipofu aliyetembea na mbwa wake kila mahali. Mbwa hawa wa nasaba ya “Labrador”, ni wanene, wapole, lakini wenye utambuzi wa hali ya juu sana. Wazungu hudai mbwa ana manufaa kwetu, ikiwemo ulinzi na usalama. Kama walivyo paka na viumbe wengine. Hutumia mapanya, inzi, nk, kutafiti maradhi mengi yanayotusumbua.

David Blankett alishika dhifa nyingi ikiwemo elimu na alitimiza kazi zake sawasawa. Hadi leo baada ya miaka 28 kama Mbunge na Waziri anaendelea kuandika makala na kufundisha vyuo tele Uzunguni. Mwaka 2015 alifanywa Profesa wa Sayansi ya Siasa na kupewa shahada ya heshima ya daktari wa huduma za serikali na elimu (PhD) kupitia chuo kikuu cha Sheffield alikokulia utotoni. Blunkett (71) kajaaliwa watoto watatu wa kiume.

Sasa hilo ni la walemavu.

Na humo humo ndimo lililopo suala la mapenzi ya jinsia moja. Kwao Wazungu haki ya kufanya utakalo inangukia pia tabia au mwenendo huu. Wapo kila kipengele cha maisha. Mashoga huwa na mienendo ya kawaida.

Kikubwa kinachotutabisha Waafrika ni pale inapolazimika kufuata haki hiyo. Kwa nchi zao kuweka masharti kuwa “msipofuata hili tutafuta fedha za misaada.” Kama Ilivyofanya serikali ya Denmark wiki jana. Kukata kiasi cha dola milioni kumi cha misaada. Kwa kuwa Denmark ni taifa kubwa la pili kutusaidia ni kipigo-uchumi.

Swali la kujiuliza ni je kwanini hatuelewani na hawa masultani kuhusu mwenendo huo?

Mitazamo yetu inakinzana.

Kwao weupe mapenzi ya jinsia moja ni suala la kisiasa na kijamii. Kwetu tunaangalia kitendo, kilivyo.

Kwanza ni Waafrika wachache sana wanaofanya na hakiendani kabisa na maumbile. Kinapofanyika aidha huwa kwa nguvu (jela, shule za kulala) au kulawiti watoto taasisi za kidini, kisiri siri. Mashehe na Mapadiri; tena wachache, mahayawani waliojificha ficha. Sisi wamatumbi hutathmini uovu wake.

Weupe hawa hawazingatii kuwa teknolojia ya mitandao imechangia kueneza sinema za ngono (“Porno”) na kuwahadaa vijana kuwa kitendo hicho ni cha kuvutia. Hawazingatii kuwa wapo wanawake walioshaharibiwa kiafya. Au watoto wagonjwa sana baada ya kubakwa au kulawitiwa, kihivyo. Je ikiruhusiwa kuwa tendo kawaida la ndoa (na eti furaha) si litawapa mashetani hawa kisu kilichonolewa? Hapo kiutamaduni ndipo hatuelewani na hawa wenye shilingi za kigeni.



Columnist: mwananchi.co.tz