Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

KITABU CHA WIKI: Mbinu za kupanga malengo

32157 PIC+KITABU TanzaniaWeb

Tue, 18 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tunapoelekea kuufunga mwaka 2018 nimeonelea tukiangalie kitabu kiitwacho ‘Upangaji wa Malengo”

Kwa Kiingereza ambayo ndiyo lugha ya kitabu, waandishi wamekipa jina la ‘Goal Setting’. How to create ana action plan and achieve your goals.

Tunashauriwa kuwa kila inapofika mwishoni mwa mwaka ni wakati mzuri sana wa kuweza kujitathimini yaani wapi ulipofikia tangu mwaka umeanza hadi unakwisha, je umeweza kuyakamilisha malengo yako yote?

Je, ni kwa kiasi fulani? au hukuweza kabisa kufanya chochote kati ya yale yote uliyopanga kwa mwaka husika?

Kitabu hiki cha Upangaji Malengo kilichoandikwa kwa pamoja na waandishi na wataalamu nguli wa masuala ya mipango na mikakati Susana Wilson na Michael Dobson kinasisitiza umuhimu na jinsi ya mtu kuweza kupanga malengo yake yoyote yale katika maisha na hatimaye kuyafanikisha ipasavyo.

“Kwa nini basi baadhi ya watu mara nyingi huonekana kukamilisha vitu kuliko wengine”? Jibu ni moja tu, wanajua jinsi ya kupanga malengo na kuyafuatilia kwa karibu kabisa.

Kitabu hiki kinaonyesha kwa vitendo jinsi ya kuweza kufikia malengo yoyote yale mtu ambayo anakuwa amejipangia, kitabu kinafundisha njia na mbinu mbalimbali za kuweza kufikia malengo yako, na kuonyesha mbinu zenye nguvu ambazo mtu anaweza kuzitumia katika kupanga malengo yake, kupanga mipango, kupata rasilimali na nguvu ya lazima ili kuweza kufanikisha malengo hayo.

Kitabu kinaonyesha jinsi ya; kufanyia kazi malengo husika kwa umakini, kugundua tatizo na kulitatua, kuwa na tabia chanya au kuweza kubadili tabia fulani, kuweka vipaumbele na kuvifanyia kazi kwa pamoja.

Waandishi hawa wanasisitiza kuwa ili kuweza kufanikisha lengo inatakikana kufanya kazi kwa bidii na kuheshimu lengo ulilojiwekea. Kiujumla kitabu hiki kinampa msomaji mbinu mbalimbali za kuweza kufikia lengo lake alilojiwekea.

Ikumbukwe kuwa suala la uwekeaji wa malengo na hata kuyatekeleza kwa wale wanaofanikiwa kufanya hivyo, ni changamoto kubwa kwa Watanzania wengi.

Kitabu hiki kinaweza kuwa msaada mkubwa kwa yule anayetaka kuanza mwaka mpya akiwa na mtazamo mpya wa kimalengo.



Columnist: mwananchi.co.tz