Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

KIJIWENI LIVE : Mikusanyiko inahusu na vikao vya wachawi usiku?

102448 Kijiwen+pic KIJIWENI LIVE : Mikusanyiko inahusu na vikao vya wachawi usiku?

Tue, 14 Apr 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

SASA hivi agizo ni kukwepa mikusanyiko isiyo ya lazima ili kuzuia kuenea kwa mambukizi ya ugonjwa wa Covid-19, unaosababishwa na virusi vya SARS corona 2.

Kijiweni kuna swali; kama wachawi wataendelea kukusanyika usiku kwenye vikao vyao, hawataeneza maambukizi?

LUQMAN: Ukoo wenu una matatizo sana. Mnashindwa kujua dunia imezingirwa na janga la Covid-19, mnashindana kutoa nyimbo na kuporana views YouTube. Hivi nyie vipi buana?

DK LEVY: Hebu kaa kimya wewe ama umerogwa nini. Wanaleteana fitina mpaka You Tube na kutambulisha wasanii wapya kwenye vicoba vyenu. Hii akili au matope? Hata hamjui mazingira yakoje?

LUQMAN: Huwa unapata muda wa kushauriana na ndugu zako kweli? Badala ya kuimba nyimbo zenye maudhui ya wakati uliopo, mnaimba mapenzi. Si ulisema Alikiba ndio mdogo wako mwenye busara? Ni busara gani za kutuimbia Dodo wakati huu wa Covid-19? Ulisema Diamond ndio mdogo wako mwenye kujua timing za biashara. Ni timing gani ya kumtambulisha msanii mpya WCB kipindi hiki Covid-19 imechachamaa?

DK LEVY: Mimi ni mwanasiasa mwenye hekima. Mtu mzima akivuliwa nguo huchutama. Niwie radhi kwa kukuamisha katika upuuzi ule. Lakini, nina shaka na mambo yanavyokwenda huko.

Pia Soma

Advertisement
Huko Konde Boy naye kaja na moto. Angalia Kichuya, Ajibu, Dilunga na Mzamiru namna walivyorogwa na ‘ulozi’ wa Kimakonde toka kwa mtoto wa Msumbuji yule.

Hawana namba tena pale Msimbazi. Watu wanaahirisha ndoa na jando, watu wanaahirisha safari na mapenzi, watu wanawaza kuahirisha uchaguzi mkuu. Wao wanatuletea ngoma mpya na kutupiana shombo huko mitandaoni.

LUQMAN: Yule demu ulimuuliza “una boyfriend?” Akajibu “kwa hapa Dar sina.” Nataka nijue naye amerogwa na uchawi gani? Kwanza kipindi hiki wachawi wanaroga kweli au wapo likizo? Tuwaambie wachawi watuache kwanza. Tupambane na Covid-19, na wao pia.

DK LEVY: Yule alishakufa ila sijui ugonjwa gani ulimuondoa. Ila nina shaka itakuwa kwa ajali ya bodaboda. Maana alikuwa anapenda bodaboda kuliko ‘mekapu’.

Kakipanda zile boksa na kupita mitaani kanajibinua kama kuku aliyetundikwa kwenye kabati la muuza chips. Halafu kakikwa juu ya bodaboda kanachati tu muda wote bila kujishikilia. Kalikuwa na dalili zote za kuwa Miss Bodaboda.

LUQMAN: Tatizo sasa hivi hata mtu akifa kawaida haiwezekani kwenda kujinafasi msibani, si unajua mikusanyiko imekatazwa? Mungu amuweke mahala pema, alikuwa anakupenda sana, ooh sorry, mlikuwa mnapendana sana.

Hivi unajua kama sasa hivi wachawi nao hawakutani kwenye mibuyu usiku? Nao wanakwepa mikusanyiko isiyo ya lazima. Covid-19 sio game la uzito mwepesi mwanangu.

DK LEVY: Hata mateja huwakutani kwenye masikani za bangi. Hata wale wakina dada nao barabarani wametoweka. Nzige wenyewe wameingia mitini itakuwa wachawi bana? Kama umegundua ni kwamba hata kunguru wa Zenji wametoweka. Wale kunguru weusi wale. Hawapo tena mitaani kuiba samaki na kula mizoga.

LUQMAN: Kwanza umejuaje kama wale akina dada nao wametoweka? Najua huwa husemi bila utafiti.

DK LEVY: Na tafiti hupingwa na kujadiliwa kwa tafiti kama huna tafiti hustahili kujadili hii tafiti. Endeleeni kupambania wafuasi wakati jamii inalia na vita ya corona. Kwanza hivi unafahamu ufahamu wa wasanii wa Bongo na mataifa mengine? Umesikia P Diddy anafanya nini huko kwao kwa ajili ya corona?

LUQMAN: Diddy ni msanii mwenye fikra za kiuongozi, ndio maana Jumapili alifanya shoo ya Insta-Live kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwawezesha wafanyakazi wa sekta ya afya Marekani. Mastaa kibao walimuunga mkono. Oprah, Chris Brown na wengine live. Lakini main event ilikuwa Diddy na watoto wake kudensi live. Watoto wenu wa Bongo hawawezi hivyo.

DK LEVY: Safi sana. Sasa narudi kwenye suala lako mtambuka la kuhusu watu kuzagaa usiku. Unataka waendelee kuzagaa wakati hakuna wateja wa kuwauzia? Kaka corona imekuja kuondoa roho za watu na kuondoa ujinga mwingi sana duniani. Mitaani pia kulichafuka karatasi za wazee wa mikeka. Corona imeondoa ligi zote na mikeka yote...

LUQMAN: Sasa hao akina dada wa usiku walishindwa kuwa wabunifu wa kunawisha mikono wateja wao? Si wangekuwa wanatega na sanitizers?

DK LEVY: Ushaona sanitaiza zinavaliwa kama ngozi? We bwana mbona unataka kuchekesha msibani? Acha kusumbua sisi watafiti...

LUQMAN: Ila ni kweli, Covid-19 ni zaidi ya noma. Wadada wauza miili walioamua kujipa likizo kwa sasa wamepatia sana, na watakaokaidi shauri yao. Tuache hayo, hivi utafiti wako umegundua nini kuhusu wachawi? Bado wanakusanyika usiku? Kwenye mikutano yao wananawa?

DK LEVY: Hakuna wanasayansi noma kama wachawi. Wakati nyie mnafunga mipaka na kuzuia watu kuja. Wachawi wanapasua anga Dar to Lagos. Lagos to Katavi kama wanatafuna biskuti vile.

Kitu pekee kinachowakwaza ni ukosefu wa maeneo ya kutua. Maendeleo huja kama mafuriko. Huleta vitu vingi na kuondoa vitu vingi Sana. Unavyojenga kila siku mnakata miti asili mjini.

Hivi sasa kwa Dar hapa kiwanja pekee walichonacho ni Mbuyu flani hivi upo Kimara Bunyokwa huko. Hilo ndo eneo pekee wanalotua. Wiki iliyopita watu wamekuta sanitaiza zilizotumika na barakoa. Tulipofanya utafiti tukagundua kuwa vifaa hivyo viliachwa na wachawi waliovitumia usiku wakati wa mkutano wao kwenye mbuyu huo.

LUQMAN: Acha kamba wewe, ina maana na wachawi wanaogopa Covid-19? Sasa sanitzers na barakoa za nini, si wangeacha mikusanyiko tu kwenye hiyo mibuyu?

DK LEVY: Mnachofeli hamjui kuwa wachawi wana vifaa vingi sana wanavyotumia katika shughuli zao. Ukisikia tunguli manaake ni mizigo mingi. Ndo maana wakielemewa na mizigo wengi hudondokea kwenye nyumba za ibada. Hujui kuwa kuna neno linasema “Njooni kwangu wote mnaoelemewa na mizigo?” Basi ndo hujikuta wameenda ‘automatikale’. Vile vifaa vina matumizi yake. Kwa wanasayansi Kama wale hawawezi kushirikiana kutumia vifaa vyote vile bila kupaka sanitaiza.

Isitoshe katika mikusanyiko yao kuna wachawi kutoka kila pande ya dunia. Tambua kuwa wachawi wanatumia ‘redio koo’ kawasiliana usiku kwa usiku.

Columnist: mwananchi.co.tz