Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

KALAMU HURU: Hili la uchaguzi tuweke hebu breki kidogo

60300 Elius+Msuya

Thu, 30 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kila uchaguzi ukifanyika CCM inashinda kwa kishindo. Tangu mfumo wa vyama vingi uliporejeshwa na uchaguzi wa kwanza kufanyika mwaka 1995, CCM imekuwa ikishinda.

Huenda CCM inapendwa sana. Huenda pia imeleta maendeleo makubwa kiasi cha kupendwa kiasi hiki. Huenda pia hakuna vyama mbadala vyenye sera nzuri zenye kuwavutia wapiga kura. Lakini lililo dhahiri ni kwamba yapo malalamiko ya muda mrefu kwamba hakuna mfumo wa haki wa uchaguzi kutokana na upungufu uliomo kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

Mwanzoni mwa miaka ya 1990 Tume ya Jaji Francis Nyalali kutoa ripoti yake ilitoa mapendekezo ya kufanyika mabadiliko ya Katiba ili iendane na mfumo wa vyama vingi.

Hata hivyo, kilichofanyika ni marekebisho tu ya vifungu vya Katiba vilivyotambua Tanzania kama nchi inayofuata mfumo wa demokrasia ya vyama vingi na mengine ambayo hayawezi kuifanya demokrasia kushamiri.

Kwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano, Rais anayo mamlaka ya kuteua viongozi wa majeshi ya Ulinzi na Usalama, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, majaji na viongozi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuanzia mwenyekiti, makamishina na mkurugenzi wa uchaguzi.

Kwa hiyo NEC inawajibika kwa Rais ambaye pia ni hugombea urais. Pia Rais anateua wakurugenzi wa halmashauri za wilaya, manispaa na majiji ambao pia husimamia uchaguzi.

Pia Soma

Wasimamizi hao wanapaswa kutekeleza majukumu yao kwa kutii katiba na bila shaka maelekezo ya aliyewateua. Hapo ndipo ugumu wa kazi ulipo.

Ndiyo maana Mahakama Kuu hivi karibuni imetoa hukumu inayozuia wakurugenzi wasiwe wasimamizi wa uchaguzi. Serikali tayari imeeleza nia ya kukata rufaa, tusubiri tuone matokeo.

Wapo wanaotetea mfumo huo wakisema hata wabunge na madiwani walioshinda upinzani walitangazwa na wakurugenzi haohao, lakini tumeshuhudia vurugu nyingi wakati wa kutoa matokeo pale upinzani unapoonekana kuwa mkubwa dhidi ya CCM.

Wakurugenzi wanaogopa kufukuzwa kazi kwa kumtangaza mpinzani kuwa mshindi na hao wanaowatangaza wanafanya basi tu kwa shinikizo la umma, lakini kwa hofu.

Tumesikia pia malalamiko ya wapinzani hasa katika chaguzi za marudio kwamba wakurugenzi walikuwa wakiwakimbia ofisini kukwepa kupokea fomu zao za kugombea, ili wagombea wa CCM wapite bila kupingwa.

Pia, wagombea wengine wamekuwa wakienguliwa kwa madai ya kushindwa kukidhi matakwa ya ujazaji fomu, jambo ambalo halijawahi kumtokea mgombea yeyote wa CCM.

Hukumu ya mahakama imeibua hoja kwamba hawa wakurugenzi ni makada wa CCM, tena wengi wao walishagombea ubunge majimboni wakaanguka.

Columnist: mwananchi.co.tz