Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Inakuwa vipi wanamichezo wasianzishe miradi yao?

9460 Goshashi+allan TZWeb

Mon, 18 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Wanamichezo ni watu wa kuigwa katika jamii, ni watu muhimu sana. Ndiyo, ni watu ambao wamefundishwa nidhamu kwa kiwango cha juu kwa sababu makocha wanapowafundisha ujuzi huwa wanahakikisha wanawafundisha umuhimu wa nidhamu katika maandalizi yao ili wapate wanayoyatarajia katika mchezo husika.

Ndiyo, wanamichezo ni watu wa kuigwa katika jamii kwa sababu wanafanya kazi yao kwa bidii.

Mwamichezo anapokuwa kwenye mazoezi, kocha wake humfundisha kufanya kazi ya mchezo husika kwa bidii ili kufikia kiwango cha juu katika mchezo huo.

Ndiyo, wanamichezo ni watu wa kuigwa katika jamii, pia ni muhimu kwa sababu ni watu wa kujitoa kwa dhati katika mchezo wanaoucheza na kutoa mchango kwa timu yao. Kwa kufanya hivyo, wanamichezo huacha mambo mengi kama kukaa vijiweni na marafiki zao, kushiriki katika starehe na mambo mengi mengine. Wanamichezo hufanya hivyo ili kujitoa kwa dhati katika mchezo kwa ajili ya kuwa na ujuzi mzuri na kuleta furaha kwa mchezo husika kwa wale watakaowatazama wakiucheza.

Ndiyo, wanamichezo ni watu wa kuigwa katika jamii na muhimu kwa sababu ni watu wanaofundishwa kushirikiana, kufanya kazi kitimu ili kupata mafanikio.

Kwa hiyo wanamichezo ni watu ambao wamefundishwa misingi ya umoja.

Ndiyo, wanamichezo ni watu wa kuigwa katika jamii kwa sababu wamefundishwa kuna kupata na kukosa au ninaweza kusema wamefundishwa kushinda na kushindwa. Wamefundishwa jinsi ya kufurahia ushindi wao bila kumdharau mpinzani wao. Wamefundishwa kutobweteka kwa mafanikio waliyoyapata katika mechi moja bali kuangalia mafanikio watakayoyapata mwisho wa mashindano. Pia, wamefundishwa kukabiliana na hali ya kushindwa katika mashindano au kukabiliana na hali ya kushindwa kufikia malengo yao. Wamefundishwa kuwa kushindwa ni jambo la muda mfupi kwa hiyo wanatakiwa kuboresha kazi zao ili kupata mafanikio wanayoyatarajia na siyo kudharau wengine.

Ndiyo, wanamichezo ni watu wa kuigwa katika jamii na muhimu kwa sababu wamefundishwa kupanga malengo yao na kuyapigania. Inafahamika kuwa watu wenye mafanikio ni wale waliopanga malengo ya muda mfupi na yale ya muda mrefu na kuhakikisha wanayakamilisha. Mwanamichezo huwa anafundishwa kuwa haijalishi kama ana kipaji au ujuzi mkubwa anachotakiwa ni kutimiza malengo.

Ndiyo, wanamichezo ni watu wa kuigwa katika jamii kwa sababu wanafundishwa thamani ya mazoezi na maandalizi kwa ajili ya kufikia malengo yao iwe binafsi au kitimu. Wanamichezo wanafundishwa kuwa uzoefu mzuri wa mafanikio hupatikana katika maandalizi sahihi. Pia, hufundishwa kuwa wanashindwa kwa sababu hawana umakini katika muda wanaouweka katika mazoezi yao.

Ndiyo, wanamichezo ni muhimu katika jamii kwa sababu hufundishwa jinsi ya kukabiliana na shida au taabu. Hili ni suala la akili ambalo hufundishwa wanamichezo ili kukabiliana nalo wakati wa mazoezi na katika mashindano.

Kwa kutazama sababu zote hizo zinazoonyesha wanamichezo ni watu wa kuigwa na pia ni muhimu katika jamii, inashangaza kuona hapa nchini hawathaminiwi, wanadhulumiwa na viongozi wa michezo nchini, Serikali haiwathamini inavyotakiwa, pia makampuni nchini na yenyewe hayajitokezi vya kutosha kuwekeza fedha kwa wanamichezo wetu.

Tunatakiwa kufahamu katika mchezo wowote mtu muhimu ni mwanamichezo na siyo kiongozi wa mchezo kwa hiyo tuwathamini wanamichezo wetu katika hali zote kwani tukiwekeza kwao na wakipata mafanikio wataanzisha miradi ambayo itatoa ajira kwa vijana wasomi na wasio wasomi.

Columnist: mwananchi.co.tz