Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Imarisha maelewano na wafanyakazi wenzako kwa njia hii

61572 AJIRA+PIC

Thu, 6 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Unajua kwamba unapoishi vizuri na watu hasa kazini maana yake unajali hisia zao, unaelewa mahitaji yao na unafanya juhudi kuhakikisha migogoro isiyo ya lazima haijitokezi.

Hilo linawezekana endapo tu, utakubali kuzidiwa kwa namna yeyote ile kiutendaji na sio ‘kutengeneza mashindano.’

Fahamu kuwa kazini watu hushindana kimya kimya kwa viwango vya elimu; utendaji wa kazi; tija waliyoiletea taasisi na mambo mengine.

 Unapoingia kwenye mfumo wa kazi, unajikuta ukiwa sehemu ya mfumo huu wa mashindano yasiyo rasmi, bila kujua.

Ukikubali kuingia kwenye mashindano haya, utajitengenezea mazingira ya kupishana na watu bila sababu.

Utajikuta ukiongea kama mtu anayejua kila kitu. Utashauri mahali ambako ushauri wako haujaombwa. Utafanya mambo kwa papara ili tu uonekane unaweza.

Pia Soma

 

Kujifunza mengi zaidi kuhusu ajira, pata nakala yako ya Jarida la Ajira kwa kununua gazeti la Mwananchi kesho

Columnist: mwananchi.co.tz