Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Hizi ndizo rangi sahihi zinazofaa kwenye chumba cha wakuu wa familia

83266 Rangi+pic Hizi ndizo rangi sahihi zinazofaa kwenye chumba cha wakuu wa familia

Sun, 10 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Rangi sahihi zitakifanya chumba cha wakuu wa familia kama mahali patakatifu. Kuchagua rangi kwa ajili ya kupaka chumba cha wazazi (master bedroom) ni moja kati ya hatua kubwa unazochukua wewe mwenye nyumba za kutengeneza mahali binafsi. Chaguo lako lina-takiwa liendane na muonekano wako kwa jinsi ya mtindo wako wa kupamba.

Kwa kuwa kwenye nyumba nyingi za kisasa chumba cha wakuu wa familia ni kikubwa kuliko vyumba vingine, una machaguo mengi na unaweza kuchanganya rangi tofauti kwenye kuta nne za chumba hiki ile kuleta muonekano wa kipekee.

Kama chumba cha wakuu wa familia kimeungana na bafu na seh-emu ya kuvalia inakubidi kuweka mpangilio wa rangi kwenye mae-neo hayo yote. Hii haimaanishi kuwa rangi ya chumbani na bafuni zinapaswa kufanana, bali inamaani-sha zinapaswa kushirikiana. Kuchu-kua rangi moja kutoka sehemu moja na kuleta mguso wake kwenye sehemu nyingine kutatengeneza chumba cha kuvutia.

Fikiria mandhari unayotaka kuitengeneza chumbani. Wenye nyumba wengi wanataka mand-hari tulivu ya rangi nyepesi. Japo hii haimaanishi kwamba rangi za kuwaka au nzito hazina nafasi kwe-nye chumba chako. Kama unadhani unazipenda rangi hizi (za kuwaka na nzito) basi fanya kuchanganya kuta na zile tulivu na nyepesi bada-la ya kupaka rangi moja chumba kizima.

Mara baada ya kuamua ni rangi zipi unataka kupaka, kinachofuata ni kufikiria jinsi gani unataka kuzitu-mia. Kama unataka rangi ya kuwaka kwenye chumba chako fikiria kijani. Je, unaipenda kijani? Kijani kama cha tufaa (apple) kina nadharia ya kuwaka na tulivu ambapo kijani hiki unaweza kukichanganya na rangi tulivu kama vile krimu na nyeupe. Vile vile bluu ya mawingu nayo ni tulivu na laini kwa chumba cha kulala. Kuna jamii nyingi za rangi ya bluu nyepesi kwa ajili ya kuta za chumba cha kulala endapo hutaki ile bluu nzito.

Bluu nyepesi zinafanya vizuri zikichanganywa na kahawia endapo nia yako ni kuchanganya nyepesi na nzito. Laa kama unataka kuchanganya nyepesi kwa nyepesi basi nyepesi ya bluu inaendana na nyeupe. Usishangae kwa nini mawingu yanapendeza! Vile vile bluu na kijani nyepesi zinapendeza zikitumika pamoja.Kama nyekundu ndio rangi unay-opendelea zaidi, unaweza kuitu-mia kwenye chumba cha kulala, ila kwa tahadhari.

Nyekundu inaleta mhemko na ikiwa nyingi inaweza kuchosha mwili. Ama chagua nyekundu iliyofi-fia au paka kwenye ukuta mmoja tu, ule ukuta wa tendego (ubao wa kichwani mwa kitanda) au ule wenye dirisha kubwa, ili mwanga upunguze makali ya rangi. Kuta tatu zilizobakia paka nyepesi ya kati ya zilizoainishwa hapo juu.

Dondoo ya nyekundu inatumika vile vile kwa njano na chungwa. Hata nyeusi inawezekana kwenye chumba chako cha kulala ila kuwa makini kuichanganya na nyeupe na utaratibu ni ule ule wa kuipaka kwenye ukuta mmoja tu kama ili-vyoainishwa kwenye nyekundu.

Columnist: mwananchi.co.tz