Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Hivi ndivyo Rushwa ya ngono inavyoua vipaji muhimu kwa Taifa

76396 Rushwa+pic

Thu, 19 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mhadhiri hayuko tayari kumpa mwanafunzi alama anazostahili kwa sababu amekataa ombi lake la kumtaka wakutane faragha. Kwa kushindwa kufanya hivyo anafelishwa.

Upande mwingine mwanafunzi anaonekana amepata matokeo mazuri kwa kuwa alitekeleza haki ombi la mwalimu kwa kumpa anachotaka na mwishowe mambo yake yakafanikiwa.

Haya ni baadhi ya mambo yanayochukua nafasi kwenye taasisi nyingi za elimu, ni malalamiko ambayo yamejenga usugu kwa sasa. Kwa kifupi hii ni rushwa ya ngono.

Ukiacha kwenye taasisi hizo, rushwa hii pia imechukua nafasi katika maeneo ya kazi, waathirika wakubwa wakiwa wanawake. Bila kumpa bosi anachotaka basi unaweza kuwa na maisha magumu kazini au kupoteza kabisa kazi yenyewe.

Hilo ndilo lililomtokea Nema Gabriel (si jina halisi), binti huyu wa miaka 23 amelazimika kushiriki ngono na wanaume wawili ili apate kazi ya uhudumu wa bar.

Wa kwanza ni aliyemueleza kuwa kuna sehemu anahitajika mhudumu. Kwa kifupi ndiye aliyempa taarifa za kibarua hicho ambacho kwa wakati huo alikihitaji mno ili kumpatia chochote.

Pia Soma

Advertisement
Mtu huyo alimweleza kuwa kazi ipo ila akampa sharti kuwa ili ampeleke sehemu husika hana budi kushiriki naye ngono.

Ili kupata undani wa habari hii pata nakala ya Gazeti la Mwananchi Alhamis ya septemba 19, 2019.

Columnist: mwananchi.co.tz