Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Hatua za kuchukua unapohisi ajira yako haikufai

Fri, 23 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Huenda umechoka na kazi uliyonayo. Unawaza ufanyeje kupata kazi ya ndoto zako lakini huna namna. Kwa upande mwingine inawezekana unaipenda kazi yako na unajituma sana kazini lakini moyoni mwako unajua kabisa unachokifanya sicho. Unafanya kazi kwa sababu tu huna namna nyingine ya kuendesha maisha yako. Ungekuwa na mbadala pengine ungeacha kazi.

Mambo mawili muhimu ya kuzingatia. Kwanza, kuna dhana imejengeka kuwa maamuzi ya kazi ni tukio linalofanyika mara moja. Kwamba unapoamua ufanye kazi gani, labda baada ya kuhitimu chuo, basi huruhusiwi kufanya makosa. Lazima uchague inayoendana na vitu unavyovipenda na ukishakosea, ni vigumu kurekebisha makosa.

Hata hivyo, tukiwa wakweli, si watu wengi hufikia ndoto zao kirahisi. Kwamba umesoma kozi sahihi chuoni, kisha unaanza na kazi sahihi unapoingia kwenye soko la ajira, huu hauwezi kuwa uhalisia wa watu wengi. Hili linatuleta kwenye mtazamo wa pili.

Hakuna kazi unayoweza kuiita si sahihi. Kazi yoyote ile halali inaweza kuwa sahihi ukiweza kuwa na mtazamo chanya. Tukiamua kutumia mtazamo huu, maana yake ni kwamba kila kazi unayoifanya ina mchango wake kukuza kuelekea kwenye wito wako.

Hata pale unapojisikia kama mtu aliyepotea, hiyo inaweza kuwa ishara ya kukutaka ujiongeze ukuze ajira yako.

Katika makala haya, tunaangazia baadhi ya viashiria vya kupotea njia kwenye ulimwengu wa ajira na namna vinavyoweza kuwa kichocheo muhimu cha kufanya maamuzi yatakayobadilisha kazi yako.

Hupati utoshelevu

Kama unafanya kazi na hujisikii kuridhika kuna mawili. Inawezekana kweli unafanya kazi isiyolingana na malengo uliyonayo na hivyo tunaweza kusema umepotea. Lakini kwa upande mwingine inawezekana tatizo linaweza lisiwe kazi bali mazingira mabaya ya kazi. Hapa kuna masuala kama uongozi usiotambua juhudi zako, kutokupanda cheo/daraja, maslahi yasiyotosha, kukosa ujuzi, kujilinganisha kupindukia na mambo kama hayo.



Columnist: mwananchi.co.tz