Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

GOZI LA NG'OMBE: Morrison na Luis si maajabu

98536 Luis+pic GOZI LA NG'OMBE: Morrison na Luis si maajabu

Tue, 10 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tarehe nane Machi pengine siku ambayo wapo watu walioweka kwenye kumbukumbu zao kutokana na matokeo yake.

Pengine wapo wanawake ambao ilikuwa siku nzuri kwao kwa sababu walipata burudani ya kitaifa ya timu mbili kubwa katika siku yao mahususi na inawezekana kabisa inaweza isijtokeze tena kwa kipindi kirefu kwelikweli.

Lakini kulikuwa na kubwa kuliko siku ya wanawake na badala yake kila mmoja aliingia uwanjani kutazama miguu ya Morrison na ile ya Luis Miquossine.

Kwa mara ya kwanza kulikuwa na “mzuka” uliobebwa na wachezaji wa kigeni kutoka pande zote mbili.

Sahau kuhusu matokeo ambayo mitandao imeshayazungumza kwa kiwango kikubwa kiasi kwamba kila mmoja kawamba ngoma kwa kuvutia kwake.

Kuna jambo moja kubwa la msingi la kutazama kutoka kwenye klabu zote mbili ambazo kwa kila mmoja na nafasi yake inaamini kuwa inastahili kutuwakilisha kwenye michuano ya kimataifa ya CAF.

Pia Soma

Advertisement
Simba wakiamini watatwaa ubingwa na kwenda klabu bingwa huku Yanga wakiwa na nguvu kubwa upande wa Kombe la TFF ili waweze kushiriki mashindano ya shirikisho.

Suala pekee ni kuwa je tupo tayari au tuna timu imara kweli? Yanga wanaamini hawana timu imara kupindukia kwasababu wamepitia masahibu mengi kabla ya mchezo huu tangu kipindi cha Zahera.

Wanaamini wanahitaji kutumia fedha za “GSM” vyema ili kujipanga kwa ajili ya msimu ujao. Simba wao wanaamini wana timu, wana uwezo na wana mdomo unaowatosha kuwa timu kubwa barani Afrika.

Hata hivyo kila nikitazama undani wa kiutendaji kidogo nakumbuka “Twiti” ya Mo kuhusiana na mishahara na nawaza wachezaji waliotimuliwa wa Yanga.

Klabu zote zina timu za kucheza na Ruvu Shooting na zikawaogopa hususani wakishaanza mdomo dhidi ya mwamuzi Martin Saanya lakini bado hatuna timu ya kuifunga Al Ahly au Mamelodi Sundowns.

Timu zote zina fedha kwa sasa lakini hazina mboni ya mbali ambayo itawaweka kwenye ramani ya dunia na kuamua kuwapa ufalme wa ukanda wa Afrika na pengine Watanzania tukaota ndoto ya kwenda kwenye michuano ya dunia ya klabu kwa sababu inawezekana.

Inawezekana kabisa fedha ya GSM ikaipa Yanga ufalme mkubwa na ni jambo la msingi kwa MO kufurahi badala ya kulalamikia wingi wa fedha anazotoa kulipa wachezaji.

Timu zote zimeanza kunufaika na biashara ya wachezaji wake japo kwa uchache kutokana na thamani ya nembo zote kuanzia kwenye jezi na udhamini lakini bado hakuna macho sahihi ya usajili wa wachezaji wa kutupeleka mbali kiushindani.

Kelele za Morrison na Luis zinaniaminisha kuwa tuna uhaba wa watu wa ufundi kuweza kupata vipaji vya aina hii kila mara na ndio maana hapa tunawaona lulu ambayo haijatokea kwa siku nyingi sasa.

Hii ndio sababu ambayo hatukuwahi kuishi bila Okwi pale Msimbazi na Niyonzima ni pengo ambalo halizibiki pale Jangwani, hatuwezi kupata wachezaji sahihi zaidi ya kubahatisha.

Umefika wakati fedha ziingie kwenye mifuko sahihi ya wachezaji wanaokuja nchini. Lazima uje wakati ambao vikosi hivi vikipangwa iwe ni mchakamchaka katika kila nafasi hususani kwa wachezaji wa kigeni ambao tunaamini wana mfano mkubwa wa kufuatwa na wachezaji wetu wa ndani.

Bado nina imani kubwa kuwa mifumo ya mabadiliko ambayo klabu hizi zinapitia inaweza kuwa baraka kubwa kwa sababu ibeba macho na matamanio ya uwekezaji na kutengeneza faida lakini bado nahisi tunahitaji mabadiliko makubwa kwenye watu wa ufundi ambao wanatuletea wachezaji.

Tunahitaji kuwa na imani Chama, Luis, Kagere, Tshishimbi, Niyonzima na Morrison sio maajabu kuwepo nchini ni lazima wawepo kila mara.

Dunia inasonga kwa kasi kwenye suala la uwekezaji katika idara ya ufundi kwenye michezo na kila timu inakula kulingana na urefu wa kamba yake.

Kama huna fedha nyingi basi ingia machimboni na chukua madini uyasafishe ili yang’are nyumbani kwako.

Kama una fedha basi unaweza nunua kwa walioingia machimboni na kung’arisha madini kisha wao wakanufaika na fedha zako.

Kila timu ina staili ya kuchagua ilimradi maisha yaendelee na tusistuke na namna Morrison anavyoganda juu ya mpira. Tuna uwezo wa kufanya makubwa na hawa wasionekane kama wana maajabu yoyote.

Columnist: mwananchi.co.tz