Thu, 6 Feb 2020
Chanzo: mwananchi.co.tz
Sehemu kubwa ya uzuri wa muonekano wa nyumba ni rangi yake. Haijalishi ukubwa wa eneo unalotaka kupaka rangi bali kupata fundi sahihi itaokoa muda, nguvu na pesa zako kwa kipindi kirefu kitakachofuata.
Nimeongea na Wakandarasi mbalimbali na wamesema kabla hujampa kazi ya kupa-ka rangi fundi au mkanda-rasi anayekidhi vigezo vyako, hakikisha yafuatayo:
Ni muda gani fundi huyo amekuwa katika kazi hiyo? Hakikisha kuwa unampa kazi fundi ambaye ameshakuwa kwenye kazi hiyo kwa miaka miwili na zaidi.
Wafanyakazi
Je, huyo fundi/mkandarasi unayetaka kumpa hiyo kazi ana wafanyakazi wake? Kazi ya kupaka rangi ukuta inahi-taji hatua nyingi za maandalizi ya ukuta kabla ya rangi ya mwisho kwa hivyo inahitaji nguvu kazi kubwa na ifanyike kwa muda mfupi ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea kwa mfano ujio wa mvua na kadhalika.
Pia Soma
- LIVE: KINACHOENDELEA KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA SHERIA TANZANIA, RAIS MAGUFULI MGENI RASMI
- Takukuru yaondoa tisa ardhi Dodoma
- Mahakama Tanzania yadaiwa ‘chaka’
Ni vyema kuhakikisha fundi unayetaka kumuajiri kwa ajili ya kazi yako ya rangi ana lese-ni ya kazi hiyo. Hii ni muhimu sana hasa pale itakapotokea ajali kwa mfano mfanyakazi wake anaweza kuanguka na kuumia vibaya au hata kusababisha kifo kama ameanguka kutoka juu ya jengo refu. Leseni itamlinda yeye na wewe kisheria kwani kazi inafanyikia kwenye eneo lako.
Taaluma
Je, fundi husika anaweza kupendekeza ni malighafi zipi zitafaa zaidi kwa ajili ya kazi yako? Awe ni mtaalam anayeenda na wakati anayejua ni rangi na teknolojia gani mpya zaidi iliyopo sokoni kwa wakati huo. Ashauri rangi na nakshi mbalimbali. Uzoefu hapa unahusika.
Makadirio rasmi
Hakikisha fundi unayetaka kumpa kazi anaweza kukupa makadirio ya muda na vifaa vyote vinavyohitajika vikiwa kwenye maandishi.
Mbali na garantii zinazo-tolewa na viwanda vya rangi, fundi rangi anatakiwa aweze kukupa garantii ya kazi yake. Maana yake ni nini? Ni kwamba fundi atapaka rangi kipindi cha kiangazi, anamaliza kazi yake na inaonekana kuvutia kabisa machoni.
Lakini mvua zikianza mwezi mmoja au wiki kadhaa baadaye unaweza kushangaa ukuta wa nje ulioloa maji ya mvua rangi yake inavimba malengelenge na inabanduka eneo kubwa. Sasa hapo sababu inaweza kuwa huenda fundi hakusimamia wafanyakazi wake vizuri na kwa hivyo wakapaka rangi ukuta wenye vumbi.
Ama wakati wa kuchang-anya malighafi zinazohitajika vipimo havikuzingatiwa matokeo yake rangi inabaduka chini ya mwezi mmoja. Kwa suala kama hili ndipo tunaposema ni vyema kuwa na fundi mwenye uwezo wa kugarantii kazi yake hata kama ni kwa miezi mitatu tu.
Gharama
Kwa asili, gharama ni suala linalotiliwa mkazo kwenye kazi nyingi. Kupata fundi wa bei nafuu kisiwe ni kigezo chako namba moja. Unataka kupata fundi mwenye ujuzi, uzoefu, leseni, makini kwenye suala la usalama na mchapa kazi.
Ni ukweli kuwa mtu wa hivi hatakuwa wa bei chee. Na hata hivyo hatakiwi kuwa wa gharama ya juu zaidi kwamba eti ndio atafanya kazi nzuri. Cha muhimu tu hakikisha haumpi fundi rangi kazi kwa kuangalia bei yake. Tafuta gharama za mafundi watatu tofauti ili ulinganishe.
Columnist: mwananchi.co.tz