Michezo ya kubahatisha ni kati ya sekta zinazokua kwa kasi Tanzania. Kwa ujumla vijana wanaonekana kuwa washiriki wakuu katika sekta hii.
Zipo aina mbalimbali za michezo hii na kampuni kadha wa kadha zinazojihusisha nayo. Pia kuna sheria, sera na miongozo rasmi ya Serikali na mamlaka rasmi zinazosimamia sekta hii ikiwamo utoaji wa leseni mbalimbali.
Kati ya mambo yanayotokea katika sekta hii ni pamoja na ushindi wa kawaida na mkubwa kwa wachezaji. Kuna haja ya elimu kwa wachezaji watarajiwa, wachezaji halisia na washindi wa michezo hii.
Kati ya maeneo yanayohitaji elimu kwa upande wa washindi ni usimamizi bora wa fedha hasa zinapokuwa fedha nyingi kwa watu ambao hawajawahi kushika kiasi kikubwa.
Kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya michezo na maendeleo ya uchumi. Michezo hutoa ajira, ni chanzo cha mapato ya Seriklai kupitia kodi, tozo na adhabu mbalimbali. Pia, michezo imefungamana na sekta nyingine hivyo kutoa masoko kama vile ya fedha, mavazi, chakula, usafiri na elimu.
Mjadala kuhusu uchangiaji wa baadhi ya michezo ya kubahatisha kiuchumi ni mkubwa. Hii ni pamoja na uwezekano wa wachezaji kupoteza rasilimali nyingi kama vile muda na fedha wanazotumia kucheza.
Kwa mujibu wa sheria, michezo hii inapaswa kuchangia maendeleo ya uchumi na jamii kwa njia nzuri. Haipaswi kuwa sehemu ya kupoteza muda na fedha. Pamoja na mambo mengine, mdhibiti mkuu wa sekta hii anao wajibu wa kuhakikisha heshima na kuwalinda wadau.
Katika bajeti ya 2018/19 kati ya maeneo ambayo Serikali inatarajia kupata fedha kwa kuongeza viwango vya kodi na tozo ni sekta hii.
Kubahatisha
Michezo ya kubahatisha ni sekta inayotambulika rasmi Tanzania. Pamoja na mambo mengine, ina historia ndefu nchini. Imekuwa ikisimamiwa na sheria ikiwamo ya mwaka 1967 na ya mwaka 1974.
Hadi wakati wa mageuzi ya uchumi katikati ya miaka ya 1980, mchezo mkuu wa kubahatisha ulikuwa bahati nasibu ya Taifa. Mageuzi ya uchumi yalichangia Tanzania kuhama kutoka uchumi hodhi kwenda uchumi wa soko huru chini ya sekta binafsi ya nje na ndani. \
Sheria ya uwekezaji ya mwaka 1992 ilichochea kutanuka kwa sekta mbalimbali ikiwamo shughuli za burudani kama vile michezo ya kubahatisha. Maendeleo ya sekta hii yalipelekea kuundwa kwa sera ya Taifa ya michezo ya kubahatisha na sheria iliyounda Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (TGB) kama mamlaka dhibiti.
Washindi wa michezo hii hupata zawadi mbalimbali kama vile magari, nyumba, tiketi za safari, fedha taslimu au mialiko ya kuhudhuria dhifa na sherehe mbalimbali.
Ipo haja ya kutoa mafunzo mbalimbali kwa wadau wa sekta hii kwa ujumla na baadhi ya michezo kimahususi. Umuhimu wa kutoa elimu ni pamoja na ukweli kuwa michezo ya kubahatisha ni pata potea na hujenga mazoea yanayoweza kuwa tabu kuyaacha.
Wataalamu wa takwimu wanaweza kuonyesha uwezekano wa kushinda kwa kila mchezo. Pamoja na hayo, elimu ya usimamizi mzuri wa fedha ni muhimu sana. Hii ni kweli zaidi hasa kwa washindi wa zawadi kubwa za mamilioni hasa wale ambao hawajawahi kupata fedha nyingi kwa wakati mmoja.
Haina maana kuwa washindi wote hawana elimu juu usimamizi mzuri wa fedha. Hata hivyo ni kweli kuwa usimamizi wa fedha nyingi zinazopatikana ghafla unahitaji elimu ili muhusika asijute pale fedha zinapotumika vibaya.
Utafiti unaonyesha watu waliowahi kupata fedha nyingi kutoka vyanzo mbalimbali lakini wakazipoteza kwa kukosa elimu ya usimamzi mzuri bila kuleta manufaa yaliyotegemewa kwa wahusika na jamii kwa ujumla.
Usimamzi wa fedha
Usimamzi wa fedha ni jambo la kitaalamu hasa kwa fedha nyingi. Washindi wa baadhi ya michezo ya kubahatisha hupata fedha nyingi kiasi cha makumi hata mamia ya mamilioni ya Shilingi.
Kwa sababu fedha hizi huja ghafla, bila kuwa na uhakika wa kuzipata au baada ya kufanya uwekezaji mkubwa wa nguvu, akili na mtaji, kuna hatari zikatumika vibaya hivyo kuhitaji mafunzo ya usimamzi wake. Maeneo ya mafunzo ni mengi kutegemea na uhitaji.
Kwa ujumla wake maeneo yanayohitaji elimu ni pamoja na ujasiriamali ili kubaini fursa za uwekezaji na biashara, kuwa na mpangilio wa biashara ikiwa ni pamoja na kutambua masoko, ushindani na matakwa ya kisheria.
Mengine muhimu kufahamu ni hali halisi ya sekta mtu anayotaka kuwekeza, vihatarishi vya biashara husika, umuhimu na namna ya kujitofautisha kibiashara, namna mbadala ya kuwekeza fedha zinazopatikana, maeneo ya kuwekeza kwa faida, gharama za kuwekeza na faida itakayopatikana.
Maeneo haya na mengine ni muhimu kwa sababu bila elimu, kuna hatari kubwa fedha za washindi wa michezo hii kwisha bila kufanyiwa jambo la maana.
Kuna njia mbalimbali za usimamizi wa fedha zinazotokana na michezo ya kubahatisha. Hawa ni pamoja na vyuo mbalimabli, watu binafsi na kampuni zinazochezesha michezo hii.
Kwa sababu sio rahisi mtu kuhudhuria na kulipia mafunzo kabla hajashinda, itakuwa na manufaa mapana kwa sekta ya michezo hii kuandaa mafunzo haya kwa washindi wake kama sehemu ya huduma kwa wateja.
Baadhi ya vyombo vya fedha na watoa ruzuku hutoa mafunzo ya matumizi bora ya fedha kwa wateja wao kabla ya kuwapa. Sekta ya michezo ya kubahatisha inapaswa kuiga mambo haya.

Michezo na uchumi

Elimu