Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Bocco, Mugalu kuna tatizo, tofauti ipo

Wazito Saana Bocco, Mugalu kuna tatizo, tofauti ipo

Wed, 19 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Huwezi kuupima uzuri wa jumla wa timu moja kwa kutazama michuano ya muda mfupi kama Mapinduzi Cup. Kwa kufanya hivyo unakuwa unajidanganya na kujifariji.

Ukweli ni kuwa Ligi Kuu Bara ambayo kila timu inacheza mechi 30 mizunguko yote miwili ndiyo kipimo cha uwezo wa timu na mchezaji mmojammoja.

Wazungu hutumia maneno ‘marathoni’ yaani mbio ndefu. Ligi Kuu ni safari ya marathoni, ni safari ndefu yenye kuzitaka timu kuwa kamilifu.

Nimewatazama Fiston Mayele na Makambo kwa sasa na nikawalinganisha na John Bocco na Chris Mugalu, kwa kweli wawili wa Yanga ni wafungaji wa kiwango cha juu. Hutumia vizuri nafasi chache wanazozipata. Huwatia njaa mabeki wa kati kwa muda wote wanaokuwepo uwanjani.

Vimo vyao, wepesi wao wanapokuwa ndani ya kumi na nane, hawahitaji nafasi nyingi kuimaliza mechi.

Hali hiyo ni tofauti kwa upande wa Bocco na Mugalu, ni washambuliaji wazito, hawawasumbui mabeki wa kati. Wanaweza kupata nafasi chache na wakashindwa kuzitumia.

Kama Simba wanataka kuutetea ubingwa wao huu ni wakati wa kujitathmini kwa kina. Bocco anashindwa hata kujiongeza, mpira wa kuotea unahesabika kama ni wa kuotea endapo mshambuliaji ataamua kusimama na kutoucheza (inactive).

Bocco kashindwa hata kujiongeza auachie umpite mpira wa krosi ulioelekezwa kwa Meddie Kagere! Hata baada ya kipa wa Mbeya City kuicheza penati bado Bocco akawa ni mzito wa maamuzi mpira ukiwa miguuni mwake. Ni kama vile kipa wa Yanga alivyoupangua mpira wa Sadio Kanoute ukimfikia yeye na akawa na miguu mizito.

Huo ni ukweli na lazima usemwe. Makambo na Mayele wanahitaji nafasi chache sana waimalize mechi, Bocco na Mugalu sijajua ni umri au wamepoteza kujiamini, hawana wepesi wa maamuzi wenye msaada kwa timu yao.

Columnist: www.tanzaniaweb.live