Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Binadamu anahitaji mabadiliko

48699 SEKELA+MWAMBULI

Tue, 26 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Ni vigumu sana kuweza kubadilika kutoka katika mfumo au tabia fulani na kwenda katika mfumo au tabia nyingine na hasa ikiwa ni kutoka katika kitu hasi na kwenda kitu chanya.

Hali hii inaweza kuchukua muda mrefu kwa mtu kubadilika na kukubaliana na hali hiyo, Lakini ni dhahiri kuwa mtu anaweza kubadilika kwa kujitoa na kufanya maamuzi kuwa sasa imetosha na nataka kubadilika na kuanza kuishi maisha mengine kabisa yenye faida.

Katika kitabu chake cha Keys for Change au vitu muhimu vya kuzingatia katika mabadiliko, mwandishi Myles Munroe anaelezea, kushauri na kuhamasiha na kwa kutumia busara jinsi ya kuishi maisha yako ndani ya mpango wa Mungu.

Kitabu hiki kinaangazia vitu muhimu vya jinsi ya mtu kuweza kubadili maisha yake na jinsi ambavyo unaweza kufaidika kwa wewe kuweza kubadilika. Hata kama mabadiliko ni hasi au chanya lakini ni jinsi tu itakavyoweza kukusaidia kuishi ili kuweza kukamilisha malengo yako hapa duniani.

Jinsi utakavyokuwa unapambana ili kuweza kuifuata miongozo hii akili yako itabadilika na kuwa mpya na maisha yako kubadilika, kujiamini, kuwa na furaha na kuweza kuishi maisha yanayompendeza Mungu. Mwandishi anasema mabadiliko ni kitu muhimu sana katika maisha ya binadamu, inaweza kuwa ubadilike kwa maamuzi yako wewe mwenyewe, lakini imekuwa ni vigumu sana kusimamaia mabadiliko hayo.

Munroe anasisitiza kwa kusema kuwa: “Hata ikitokea ukawa katika kipindi chochote kile cha mabadiliko na mabadiliko hayo yanakuhangaisha usijisikie kuwa uko peke yako na umeachwa , sisi wote kama wanadamu tunahitaji mabadiliko”

Mabadiliko huweza kuathiri maisha yetu tuliyokwisha yazoea, familia zetu na hata kazi zetu pia. Lakini pia mabadiliko yanayotokea kutokana na watu wengine, huweza kuathiri mtu binafsi, jamii, taifa na hata dunia kwa jumla.



Columnist: mwananchi.co.tz