Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

ANTIE BETTIE: Nashindwa kumridhisha mwenza wangu, nifanyeje?

97585 Anti+bettie ANTIE BETTIE: Nashindwa kumridhisha mwenza wangu, nifanyeje?

Mon, 2 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Habari Anti, nina tatizo na limekuwa likinidhalilisha. Ninashindwa kumridhisha mwenza wangu, tukiwa katikati ya mchezo uume wangu unauma na unasinyaa na unaweza usiamke wiki nzima. Sasa nashindwa kujua nina tatizo gani na nifanye nini?

Inawezekana kweli una tatizo, lakini unavyozidi kulifikiria ndiyo hali inazidi kuwa mbaya.

Hujaniambia lilianza muda gani na hapo kabla ilikuwaje, ndiyo maana ninachelea kusema una tatizo au la. Lakini kwa sasa nakushauri ukiingia katika shughuli achana na mawazo kuwa humfurahishi mpenzi wako, pia usitumie muda mwingi kuandaana ili uuwahi, maana ukitumia muda mwingi utaruhusu mawazo mengine na utasinyaa tena. Pia kwa ushauri zaidi unaweza kuonana na wataalamu wa saikolojia inaonekana una shida ya kisaikolojia.

Suala la kumridhisha mpenzi wako halitegemei sana kuingiliana moja kwa moja, unaweza kumridhisha kwa kumchezea kulingana na maelekezo yake. Hivyo wakati huu unapambana na hali hiyo jitahidi kumsoma mwenza wako namna ambavyo utamsaidia kumaliza haja zake tofauti na kujamiiana.

Akiwa nami anazima simu, nahisi ananizunguka.

Nikiwa na mpenzi wangu ambaye ninataka kuanza taratibu za kufunga naye ndoa anazima simu, nikimuuliza anasema haina chaji na hilo hutokea mara kwa mara. Pia sijawahi kukuta meseji hata moja katika simu yake, kila nikibahatika kuishika nakuta zimefutwa, yaani hakuna hata tangazo la kampuni ya simu.

Pia Soma

Advertisement
Je, niendelee na utaratibu wa kumuoa? Maana nahisi ananizunguka.

Hapo jifikirie mara mbili, kwa nini anazima simu kila anapokuwa na wewe? Huo ni upande mmoja, lakini upande mwingine inawezekana hataki matatizo kwa sababu simu ni chanzo cha kuvunja uhusiano wa watu wengi. Inaweza kuingia meseji isiyoeleweka ikawavuruga. Narudi kwako una sababu gani zinazokufanya kila unapokutana na mchumba wako kushika simu yake? Unajua simu ni hatari sana katika mahusiano, huna lingine la kuzungumza naye zaidi ya kunyatia simu yake?

Simu ya mkononi maana yake kila mmoja ana yake. Kushika shika ya mwenzako ni kuonyesha hujiamini na yeye humuamini.

Suala la kufunga ndoa na simu ni vitu viwili tofauti, endelea na taratibu za kumuoa, acha kulinganisha mambo ya maana na vitu vya kawaida.

Mwanamke mwenye mambo mengi utamjua siyo kwa kuzima simu bali kwa matendo yake.

Jiamini kama mwanaume na kama kweli anakupenda hawezi kufanya mambo ya kipuuzi. Kumbuka anayechepuka haiwi rahisi kumkamata lazima atakuwa na mbinu za medani kuficha uovu wake, kuendekeza mambo ya simu utajikuta unashindwa kumpa mpenzi wako anavyostahili unasikilizia nini kimeingia katika simu yake badala ya mwilini mwake.

Columnist: mwananchi.co.tz