Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

ANTI BETTIE: Tatizo mke wangu anapenda fedha nafikiria kuachana naye

78715 Anti+bettie

Mon, 7 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Nimeoa baada ya kukaa kwenye uchumba kwa miezi sita. Tatizo huyu mke wangu anapenda fedha hadi nahisi kizunguzungu.

Nilipomuoa alinikuta ninajenga kwa kudunduliza, lakini katika kipindi cha mwaka mmoja tuliokuwa pamoja kila kitu kimesimama.

Nifanyeje?

Sidhani kama hizo fedha anakuomba bila kukujulisha nakwenda kuzifanyia nini, kama anakujulisha hilo si kosa lake ni lako kwa sababu unapaswa kupima anakozipeleka na umuhimu wake. Kama anakuomba kufanyia mambo yasiyo ya maendeleo na unampa unatakiwa ujitafakari.

Pia jukumu lako kama mume ni kutafuta fedha, lakini ili zitumike vizuri mshirikishe tofauti na hapo atakuomba kila siku akijua unazo.

Hakikisha unaweka mazingira mazuri ya matumizi ya fedha badala ya kulalamika, mwambie kuwa anatumia vibaya ukimpa mifano hai na yenye mashiko ikiwamo kuzinywea pombe na marafiki, kusafiri bila sababu za msingi, kusuka nywele, kuvaa mavazi ya gharama tofauti na uwezo wenu.

Pia Soma

Advertisement
Zingatia kuwa mkeo lazima asuke, avae vizuri, anukie hilo ni jukumu lako, lakini vifanyike kulingana na uwezo wako na makubaliano yenu kama wanafamilia.

Ukimuendekeza yeye ina maana hamtasaidia familia, kubalianeni kama familia kuwa uwezo wenu wa kifedha ni huu na zinapaswa zitumike kwa mipaka hii.

Ukimuacha utakuwa umeidhulumu nafsi yake na yako kwa sababu mnapendana na fedha hazizungumzi hadi mzipe nafasi ya kuwatenganisha. Nyinyi ndiyo mnaozungumza hivyo zungumzeni jinsi ya kuzidhibiti fedha badala ya kuacha ziwadhibiti.

Anataka kuoa kwa sababu amezaa nje

Mume wangu kampa mimba binti wa mtaa jirani na familia yake imemkomalia amuoe.

Nami sitaki ukewenza anti nifanyeje?

Kwanza mumeo kakukosea kisha anataka kuoa kabisa, angetaka kufanya hivyo angekushirikisha mkakubaliana (hapa kulingana na imani ya dini, zipo ambazo zinaamini kwenye ndoa moja), si lazima kukushirikisha lakini angekuwa na sababu za msingi za kukueleza badala ya hii ya kutoka nje ya ndoa tena jirani hadi kuzaa.

Kwanza aliweke sawa hili ikiwamo kukuomba msamaha, kabla ya kuja na hoja ya kuoa. Usikubali kuachika kwa sababu hii, hakikisha mumeo anakuwa upande wako kwa kuamua kwa haki. Unaweza kukubali kumlea mtoto na si lazima kumuoa. Uamuzi wa kuongeza mke wa pili unategemea na namna mtakavyokubaliana na mumeo, kigezo kisiwe kumzalisha mwanamke, simama kama mke taratibu zifuatwe.

Columnist: mwananchi.co.tz