Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

ANTI BETTIE: Ninashindwa kujamiiana naye kwa kuwa ni mkavu sana - VIDEO

Mon, 22 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Ninapata wakati mgumu kumuingilia mke wangu kutokana na kuwa mkavu sana.

Licha ya kumuandaa halainiki.

Nifanyeje?

Pole sana. Ila sidhani kama unamuandaa vya kutosha, tofauti na wanaume baadhi ya wanawake hisia zao zipo mbali hususani anapokuwa anajilazimisha kukupenda.

Nenda kajipange upya kumuandaa, usisahau kumshirikisha mwenyewe akueleze anajisikia raha ukimgusa wapi na wapi, inawezekana unakomshika wewe siko anakoburudika.

Ukishindwa kabisa tumia mafuta maalumu ya kulainisha uke, vilainishi vipo vingi.

Pia Soma

Lakini nina imani bado hujampatia, endelea kumtafuta utampata.

Mke wangu ndiyo ana tatizo la kutozaa, kwa sababu nimempa mimba kimada

Nimeishi na mke wangu kwa miaka tisa sasa, hajapata mtoto. Niliwahi kuwa na uhusiano na binti mmoja akapata mimba yangu kwa bahati mbaya ikaharibika.

Hivyo mimi kizazi ninacho, nimebaini mke wangu ndiyo ana shida. Nifanyeje?

Achana na mfumo dume. Kwa nini unaamua moja kwa moja kuwa mkeo ndiyo mwenye shida ya uzazi ilihali hamjapima?

Kumpa mimba kimada tena iliyoharibika si kipimo kuwa wewe una uzazi kama ameweza kutoka na wewe mume wa mtu anashindwa vipi kutoka na mwingine akapata ujauzito huko kisha akakuambia ni ya kwako? Tafadhali mchukue mkeo mwende hospitali mkapime mpate uhakika nani ana tatizo na inawezekana wataalamu wa afya wakawashauri cha kufanya ili mpate mtoto.

Halafu miaka tisa ni mingi kutokuwa na mtoto, lakini michache kama mna upendo na kushirikiana kupata ufumbuzi wa suala hilo, inawezekana hata tabia na maneno yako kwake ikiwamo shutuma yanachangia kutompata.

Majibu ya wataalamu wa afya ndiyo suluhisho la familia yenu.

Anashinda na kanga ya kifua na siyo wa Uswahilini

Mke wangu anashinda amevaa kanga ya kifua kutwa nzima, kibaya zaidi unaweza kusema ni mwanamke wa Uswahilini, huyu ni wa matawi lakini sijui ana shida gani.

Nifanyeje?

Kwanza hakuna wanawake wa Uswahilini wala wa matawi, tofauti yao ni maeneo wanayoishi, yanayoendelea kati yao ni tabia ya mtu. Kama hiyo ya mkeo, licha ya kuwa matawi bado anafanya mambo ya ajabu ajabu. Mwitie shangazi au bibi yake uje uwaeleze tabia yake hiyo na namna inavyokukera, kama umeshazungumza naye na ameshindwa kukuelewa.

Pili uonyeshe jinsi ambavyo tabia hiyo inakukera kwa kuchukia ikiwezekana kwa vitendo, kwamba ukimkuta amevaa hivyo mjaribu kumkalia kimya, kasirika wazi wazi ajue kuwa hupendi

Columnist: mwananchi.co.tz