Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

ANTI BETTIE: Nina miaka 29, sijawahi kujamiiana hata mara moja

80953 Anti+bettie ANTI BETTIE: Nina miaka 29, sijawahi kujamiiana hata mara moja

Mon, 21 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Nina miaka 29, sina mpenzi, mchumba wala sijawahi kufanya mapenzi kwa sababu sina hisia.

Je, huu ni ugonjwa au huwa inatokea?

Huna mpenzi wala mwanaume ni ngumu kujua kama una hisia au huna labda kama utakuwa kiruka njia.

Lakini hata hivyo nenda kaonane na daktari wa masuala ya wanawake akupe ushauri zaidi, kwa umri wako lazima uwe na hisia kwa sababu baada ya balehe tu wasichana na wavulana huanza kutamani kuwa na uhusiano sembuse wewe una miaka 29, kuna mahali hapako sawa.

Rafiki yangu ameshindwa kunitongozea mwanamke nimpendaye

Habari Anti. Kuna binti nilikuwa ninampenda yupo karibu na mke wa rafiki yangu, hivyo nikamtuma huyo rafiki yangu aniunganishe naye. Amenikataa nifanyeje na ninampenda kwa dhati.

Pia Soma

Advertisement
Zungumza kwa nguvu halafu usikilize ulichokiandika. Hata kama ningekuwa mimi ningekataa. Unamtumia rafiki yako ambaye ana mkewe akakuunganishie kwa mwanamke, kosa la kwanza kabisa umeonyesha udhaifu si ungekwenda tu mwenyewe kama una ni naye ya dhati.

Hapa hata mkipendana ukamuoa baadaye, historia haitafutika itabaki kuwa uliunganishiwa mwanaume na shemeji yake, hivyo siku nyingine ukimpenda msichana nenda kazungumze naye mwenyewe na achana na tabia ya kutamani, jitahidi unayekwenda kuzungumza naye uwe umempenda kwa ajili ya kufanya naye maisha. Huu si wakati wa kumpenda mwanamke kwa ajili ya kutembea naye na kumuacha.

Kosa la pili ambalo ni kubwa badala ya kumtuma huyo rafiki yako aende kwa wazazi wake rasmi kama mshenga kuulizia taratibu za kupeleka posa, wewe umemtuma akuunganishie maana yake ni kamba nia yako ni kutaka muingie kwenye uhusiano kwanza.

Kama umempenda kweli mtume yule rafiki yako afuatilie taratibu zikoje kisha mkatoe posa kwao mfunge ndoa ili ufurahi naye akiwa mkeo badala ya kuruka ruka mabararani.

Columnist: mwananchi.co.tz