Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

ANTI BETTIE: Nina maumbile makubwa, nifanyeje ili nimpate atakayenimudu?

98344 Anti+bettie ANTI BETTIE: Nina maumbile makubwa, nifanyeje ili nimpate atakayenimudu?

Mon, 9 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Anti habari!

Mimi ni kijana mwenye miaka 19, kila nikiangalia maumbile yangu nayaona makubwa kiasi kwamba nashindwa kuwa na mwanamke kwa kuhofia kumuumiza. Kuna wakati hadi nalia kwa kujihurumia, sidhani kama nitapata mwanamke atakayenimudu.

Nifanyeje?

Hujapima ukaniambia ina ukubwa kiasi gani, ila unalalama tu kuwa ni kubwa hivyo nashindwa kujua nianzie wapi.

Kukata tamaa ni dhambi, unasemaje hutapata mwanamke atakayekumudu umejuaje?

Lakini ninachojua kila unachopewa unapata na namna ya kukitumia, hivyo usijifiche na kuogopa kutafuta mwanamke inawezekana kabisa kumpata anayekumudu. Unajua kama kuna wanawake wanahitaji wanaume wenye maumbile makubwa inawezekana pengine kuliko yako. Sisemi ujaribu jaribu, lakini utakayempata atajua jinsi ya kufurahia faragha. Halafu ukiishi naye kwa muda mrefu atazoea na hatataka tena kupata mwanaume asiyekuwa na maumbile kama yako.

Pia Soma

Advertisement
Pia jifunze jinsi ya kuutumia kwa sababu ikiwa kubwa haina maana umuumize mwanamke kuna namna utakavyoitumia na akafurahia faragha.

Ninaweza kusema una bahati kupata hicho ulichonacho, jipange namna ya kukitumia kwa usahihi.

Mnapokuwa faragha kinachoangaliwa ni namna unavyomuandaa, akiwa tayari amekolea maandalizi na amelegea kisawa sawa, hawezi kukumbuka kama una maumbile makubwa au madogo. Ukiona analalamika kuumia ujue ana shida nyingine au hujamlainisha vya kutosha. Hivyo fanyia kazi eneo la maandalizi, ukiwa tayari katafute mwenza wa halali.

Mpenzi wangu msiri, sijui kama ananipenda

Nina mpenzi nampenda sana, lakini yeye ni msiri hivyo nashindwa kujua kama na yeye ananipenda au laa! Kwa sababu hasemi lolote kuhusu uhusiano wetu.

Nifanyeje?

Jamani, kitendo cha kuwa na wewe kwanza kinaonyesha anakupenda, sijajua unataka afanye nini ili kudhihirisha upendo wake kwako.

Labda ungeniambia anafuata fedha na mali ulizonazo, tofauti na hapo yupo na wewe kwa ajili ya mapenzi.

Halafu mtu hujamuoa, umesema ni mpenzi wako unataka aanze kujianika kuwa anakupenda ukimuacha je? Muoe apate uhakika wa penzi lake, auweke moyo wake mahali salama, unataka ajitangazie ushindi wakati anahisi atakuja kushindwa.

Kwanza kukaa naye kiuhawara bila kumuoa kunamfanya apunguze kujiamini na ndiyo maana haoni sababu ya kukuonyesha kama anakupenda kiasi gani.

Pili unatumia vipimo gani kujua mwanamke anakupenda au hakupendi.

Bila shaka kukubali ombi lako na kuwa na wewe kwa muda mrefu ni mojawapo ya kipimo cha mapenzi yake kwako.

Nakukumbusha tu, fanya taratibu za ndoa ili mpenzi wako ajimilikishe kwako jumla.

Columnist: mwananchi.co.tz