Habari Anti! Sijui kwa nini lakini kila nikifanya mapenzi na mwenza wangu ninaumia.
Nimevumilia hali hiyo kwa miaka kadhaa sasa, naomba ushauri wako nifanyeje?
Inawezekana kuna shida kwenye maandalizi yenu kabla hamjaanza kulicheza samba. Pia inawezekana mwenzako ana maumbile makubwa tofauti na ya kwako, ingawa hili silipi nafasi kubwa kwa sababu kwa mwanaume anayejua mambo ya faragha shughuli kubwa siyo sababu anaweza kukuandaa na ukafurahia tendo.
Kutokana na suala lako kutokuwa na jibu la moja kwa moja, nakushauri mwambie mwenza wako muongozane wote kwa daktari wa masuala ya wanawake mumueleze tatizo lenu.
Daktari anaweza kuwa kwenye nafasi nzuri ya kuwashauri cha kufanya kulingana na maelezo yenu ninyi nyote.
Wakati huu unajipanga kumueleza mumeo hakikisha unatumia ushawishi wa kike kwa sababu baadhi ya wanaume wa Kiafrika siyo rahisi kuongozana nao hospitali, usimnyime tendo kwa sababu ya maumivu, mweleze ili mjue jinsi ya kukabiliana na tatizo hilo. Hospitali ni muhimu.
Pia Soma
- USHAURI WA DAKTARI: Kuwa na nguvu za kiume ni kitu kimoja na uwezo wa kutungisha mimba ni kitu kingine
- MAISHA NA UHUSIANO: Mambo muhimu kwa wake kuzingatia ili kuboresha ndoa zao -2
- Mahakama yatengua uamuzi wa msajili wa vyama dhidi ya DP
Nilikuwa nina mpenzi , nilimpenda sana na nikamshawishi anizalie mtoto, baada ya kuzaa akanikataa yaani tukaachana. Nilipomuhitaji mtoto wangu aliniambia nimpe fedha anipe mtoto, nikafanya hivyo. Baada ya miaka kadhaa amerudi anamtaka mtoto anasema tumlee pamoja.
Nifanyeje kwa sababu aliniuzia sitamani kumpa?
Hili ni suala la kifamilia zaidi, hujasema alikuuzia kwa namna gani, inawezekana alidai fidia ya kumuhudumia mtoto wakati hampo pamoja. Sibariki hilo maana ni sawa na unavyosema amekuuzia ingawa kuna baadhi ya makabila lipo kimila na lina nguvu. Ninachokushauri kama ulimchukua mtoto na unaishi naye katika misingi mizuri ili kuepusha usumbufu mkubaliane kumlea kwa pamoja. Kwa mfano unaweza kuishi naye wakati wa likizo akaenda kwa mama yake, kama unadhani huko ataendelea kulelewa katika maadili mema. Kama una mashaka na malezi ya mwanao akiwa huko kwa sababu mbalimbali waeleze wana familia wa pande zote mbili mkae mlijadili. Nina wasiwasi lakini na gia ya huyo mama wa mtoto, inaonekana anakufuata wewe kimapenzi na si mwanae uwe makini na hilo pia.