Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

ANTI BETTIE: Namuhitaji mume wa mtu muda wote na wala simchoki

68623 Pic+mume

Sun, 28 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Anti usiniseme naomba nieleweshe, nina uhusiano na mume wa mtu cha kushangaza sichoki kuwa naye, ninamuhitaji muda wote.

Isingekuwa ni msaada kwa wengine ambao hawajajiingiza kwenye uhusiano na waume za watu nisingekujibu swali hili.

Kwa faida ya wengine ninakuambia kuwa mume wa mtu, kama ilivyo kwa mke wa mtu ni sumu. Inawezekana anakosa muda wa kukaa na familia yake kwa ajili ya kukuridhisha wewe bazazi kutokana na kumng’ang’ania. Alikuambia nani kitu cha kuazima huwa kinaisha hamu. Unatamani kuwa naye muda wote kwa sababu si wako, ikifika muda anakwenda kwa mkewe na familia yake.

Wanawake muwe na huruma na mjihurumie, huu mnaofanyiwa na wanaume ni udhalilishaji, unajisikiaje unakuwa na mwanaume, unamuachia mwili wako, unampa akili yako, unamuwaza muda wote, lakini mwisho wa siku anakuaga anakwenda kwa mkewe na unajua fika kuwa hawezi kukuoa.

Kwa nini usitulie ukatafuta mwenza wako wa kudumu ukaanzisha familia yenye amani.

Unajidhalilisha na hata huyo mume wa mtu uliyenaye hakuheshimu anakutumia na ndiyo maana hawezi kumuaga mkewe kuwa anakuja kwako, bali anakuaga wewe anayekudharau kuwa anakwenda kwa mkewe.

Pia Soma

Sura yake inanivutia, tabia yake imenishinda

Ninaishi na mchumba niliyekuwa natarajia kufunga naye ndoa. Tatizo naona nimeshindwa tabia zake. Licha ya kuwa na sura na umbo la kuvutia, hana staha, anaropoka neno lolote bila kujali tupo na nani na wakati gani.

Cha kushangaza hakuwa na tabia hizi hapo awali.

Nifanyeje?

Umemuweka ndani amevimba kichwa anajua huwezi kumuacha. Sasa kabla hujaona redio ya kuzungumza chochote na kwa wakati wowote mkanye na umueleze kwa tabia zake hizo unafikiria mara mbili kufunga naye ndoa.

Usiishie kwake, kwa sababu hujafunga naye ndoa nenda kamueleze na mshenga wake, mumuweke kikao mzungumze naye.

Baada ya hapo kaa naye wiki mbili za uangalizi kama hajajirekebisha mrudishe kwao akajifunze kabla hujamuoa.

Kwa sababu haya ni mapenzi na anayependa ni vigumu kubadili maamuzi licha ya kulalamika. Sikushauri umuache, ninakushauri kuwa makini hakikisha anajirekebisha kabla hujamuoa na kujuta siku za usoni.

Mkumbushe kuwa ‘uzuri wa mwanamke siyo urembo ni tabia’.

Nahisi amenichoka

Anti nahisi mwenza wangu amenichoka, kwa sababu nikimuita kuna wakati haitiki hata kama tumekaa jirani. Anaweza kukaa wiki mbili hajala chakula cha nyumbani, wala kunigusa.

Nifanyeje?

Inawezekana kuna kitu umemfanyia kimemkera ila hujui.

Mwanaume akikuchoka hana uvumilivu hata kidogo angeshakutimua. Jambo la kufanya tafuta siku ana nafuu kidogo muombe mzungumze, wakati mzuri ni wa kupumzika mkiwa ndani wawili.

Hata kama hataitika bila shaka atakuwa anakusikia, muelewe jinsi anavyokuumiza kwa tabia yake hiyo na kama kuna kosa akueleze.

Usimwambie kwa kulalamika, kupayuka wala kulia. Mwambie ukiwa umetulia na unamaanisha unachokizungumza.

Columnist: mwananchi.co.tz