Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

ANTI BETTIE: Mwanamume wa ajabu kweli huyu, anawapigia rafiki zangu kunikashifu

47097 Pic+betie

Mon, 18 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Anti mume wangu ananikosea sana nashindwa hata nifanye nini?

Kila inapotokea tofauti kati yetu maneno yake ni ya kunikashifu na wakati mwingine anawapigia simu rafiki zangu kwa nguvu kuwapa kashifa zangu kati kati ya ugomvi wetu.

Nifanyeje?

Pole sana. Kwanza ili usimpandishe jazba kiasi cha kupiga simu kukunanga kwa marafiki zako hakikisha mnapotofautiana unakaa kimya unamuacha aseme peke yake.

Pili hili suala hupaswi kulichekea hata kidogo, mumeo kukukashifu ni tabia mbaya, anakukosea heshima mbele ya watoto na majirani pia, hivyo washirikishe ndugu zake wamkanye.

Akifanya hivyo hivi sasa usimsamehe kirejareja hakikisha kunakuwa na kikao angalau cha watu wawili, watatu wa familia kulijadili na lipatiwe ufumbuzi, hii ifanyike baada ya wewe mwenyewe kushindwa.

Mara nyingi nashauri mambo ya ndoa yamalizwe na wanandoa, lakini kwa hili inaonekana limekuzidi nguvu na mumeo ameshakuzidi nguvu ya kufanya hicho ninachokiita dharau.

Hataki kutoka na mimi, Je, ananipenda?

Nimemuoa huu ni mwaka wa nne nampenda na ninahisi ananipenda. Ila napata mashaka tunapotaka kutoka hataki tuongozane ataniambia nitangulie na atajiunga na mimi baadaye . Tuna gari moja yupo radhi akodi gari imchukue peke yake kuliko kupanda kwenye gari yangu tukaenda wote.

Vivyo hivyo hata kunapokuwa na hafla kazini kwangu hawezi kuja hata nimbembeleze vipi.

Atakuwa ananipenda kweli?

Kama amekubali umuoe na mnaishi hadi sasa bila shaka anakupenda, mwanamke hawezi kuficha hisia za kutokupenda kwa kipindi chote hicho.

Unachotakiwa kufanya ni kujichunguza kama uliwahi kufanya kitu ikiwamo kuwa na uhusiano na wanawake na mkeo akafahamu.

Wanawake wengi hususani walioolewa wamekuwa waoga kutoka na wame zao kutokana na kuogopa kuonekana vituko na vimada wao.

Hii nina uhakika nayo na inawezekana ndiyo inayomfanya asiwe na ujasiri ya kuja ofisini kwenu kwa sababu hajui hao vimada ni wa kazini kwako, maeneo mnayokwenda kutembea ndiyo maana hajiamini kuwa na wewe.

Jitafakari hilo kwanza kama limewahi kutokea ndiyo sababu ya kukosa uaminifu kati yenu.

Anza na hilo kwanza kabla ya kufikiria kama anakupenda au hakupendi.



Columnist: mwananchi.co.tz