Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

ANTI BETTIE: Mke wangu hajui Kiingereza, nifanyeje ananitia aibu

60999 Anti+bettie

Mon, 3 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Nampenda mke wangu, tatizo lake alinidanganya kuwa amesoma, nimekuja kubaini hajasoma na kibaya zaidi hajui lugha ya Kiingereza amekuwa akinitia aibu kwa wafanyabiashara wenzangu na wageni wangu ambao wengi ni kutoka nje ya nchi.

Nifanyeje?

Mudi, Mtwara

Mudi usipoteze muda mpeleke akasome lugha hiyo ni rahisi akitia nia.

Mkataze kwa sasa kuropoka ropoka maneno asiyoyajua kwa kutumia lugha hiyo. Mueleze ni jinsi gani unatamani aijue lugha hiyo kwa ufasaha ili muweze kuwasiliana na wageni na wafanyabiashara wenzako, hii itampa moyo wa kusoma kwa bidii na kuelewa.

Akielewa lugha mpeleke akasome masomo ya sekondari kwa miaka miwili (QT) kwa sababu elimu haina mwisho.

Pia Soma

Naipenda miguu yake sitaki wengine waione

Anti naomba unisaidie, mume wangu anapenda kuvaa pensi na kitu ninachopenda kutoka kwake ni miguu, hivyo natamani asivae kwa sababu naamini wanawake wengi watamzimikia.

Nifanyeje?

Jamila, Tanga

Hujaniambia kama umewahi kumkataza akang’ang’ania.

Naamini ukimwambia kuwa miguu yake inakuvutia na hutaki mwingine aione, ataacha kuvaa penzi, usipomwambia hatojua.

Lakini sidhani kama ukipendacho wewe na wengine wanakipenda, inawezekana ikawa ngumu kukubali kutovaa, hivyo amini ni wako na itabaki kuwa hivyo.

Ameshindwa kunizalia namuacha

Nimekaa na mke wangu kwa miaka minane, hajazaa na ninapata lawama kiasi cha kukorofishana na ndugu zangu.

Anti ninamuacha kwa sababu hiyo lakini bado nampenda. Nifanyeje?

Edwin, Kigoma

Usinikere Edwin, mtu mzima na akili zako unamuacha mke kwa sababu hajazaa? Wewe ni Mungu unayetoa watoto?

Achana na maneno kutoka kwa watu wengine huyo ni mkeo na wewe ndiyo una maamuzi naye.

Nendeni Hospitali mkaonane na wataalamu watawapa muongozo wa kufanya, ili kujua tatizo na namna ya kulitatua.

Utafanya nini iwapo utamuacha na kubaini kuwa wewe ndiyo una tatizo?

Simama kama baba na kichwa cha familia kulimaliza hilo, kwa amani badala ya kukimbilia kumuacha mkeo unayempenda.

Columnist: mwananchi.co.tz