Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

ANTI BETTIE: Mchepuko umenifikisha kileleni baada ya kusota miaka 11

ANTI BETTIE: Mchepuko umenifikisha kileleni baada ya kusota miaka 11

Mon, 28 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Nimeolewa nina miaka mingi, huu ni mwaka wa 11 na sijawahi kusikia raha ya tendo la ndoa . Nikaamua kuchepuka nimesikia raha hatari.

Nifanyeje ili nisikie raha hiyo nikiwa na mume wangu?

Unajua umeshajitia kilema ambacho hakitakutoka maishani, umeolewa lakini umeamua kuwa kahaba ungetumia busara kuuliza kabla hujachepuka. Jutia kwanza tendo hilo na uanze upya, inawezekana huyo uliyekutana naye ni mjanja na amejua unataka nini tofauti na mumeo anayetaka umtajie maeneo unayotaka akushike. Kuanzia sasa mwelekeze mumeo unataka akushike wapi, na kama husikii raha pia mwambie badala ya kufanya hivyo kwa hawara.

Umekosea sana kutoka nje ya ndoa na umefanya jaribio baya kufanywa na mwanamke aliyekula kiapo cha kuwa mke wa mtu.

Sasa hakikisha raha uliyoipata huko nje unaipata kwa mumeo kwa kumueleza wazi kuwa hupati raha mnapokuwa faragha, mng’ang’anie hadi uwe kero kuhakikisha anatimiza jukumu lake la msingi.

Moyoni azimia kutochepuka tena kwani kufanya hivyo kunaweza kuharibu ndoa yako na hakumdhalilishi mumeo tu, bali hata wewe, mwanaume utakayekuwa naye anakudharau ila kwa kuwa unampa anachotaka hatakuambia.

Pia Soma

Advertisement
Usidanganyike penzi la uhakika utalipata kwa mumeo na si kwingine, nje watakudanganya kisha watakupiga chini tu.

Kibaya zaidi siku hizi kuna hatari ya kurekodiwa video, kuwa makini yasije kukuta kama yaliyowakuta wanawake walioamua kujitoa fahamu.

Naota nafanya mapenzi na mtu nisiyemjua

Anti habari, nina tatizo siwezi kumaliza wiki mbili bila kuota ninafanya mapenzi na mtu nisiyemjua. Hilo linaweza kuwa tatizo gani?

Hujasema una umri gani, una mke, mpenzi au hauna ndiyo maana ninashindwa kujua unaota ndoto za aina gani.

Ungekuwa na umri wa kubalehe ningesema hizo ni ndoto za balehe ambazo huwatokea vijana wengi wakiwa kwenye wakati huo.

Kama ni mume wa mtu kuna jambo halipo sawa, hukamuliwi ipasavyo yaani unahitaji kuongezewa huduma na mwenza wako.

Jambo ninaloweza kukushauri ni kufanya sana mazoezi kunaweza kukupunguzia hali hiyo.

Kama ni kijana na hauna mwenza wako jitahidi kumtafuta ili atimize wajibu wake, tofauti na hapo utaendelea kuota hizo ndoto kwa sababu utakuwa na vitu vingi mwilini.

Columnist: mwananchi.co.tz