Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

ANTI BETTIE : Machejo yake yananivuruga hadi nabaki nikicheka peke yangu

43482 Pic+machejo ANTI BETTIE : Machejo yake yananivuruga hadi nabaki nikicheka peke yangu

Mon, 25 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Nimeoa binti wa miaka 19 na nina miaka 62. Anachonifanyia nashindwa kuvumilia na kila nikikumbuka hata kama nipo kwenye shughuli zangu nacheka peke yangu na kusisimka.

Nimetuma ujumbe huu kwako anti iwe elimu kwa wanawake wote hususani watu wazima wanaobweteka wakiwa na wenza wao. Watoto wadogo wanajua mambo jamani acheni utani.

Anti sikufichi huyu mtoto ananifanya nijihisi nina miaka 25 namna anavyoniliwaza na puta, tunakwenda taratibu lakini ninaridhika, hakika ananikata kiu yangu.

Haya kina mama salamu zenu kama hizi nimekuwa nikizipata nyingi ila leo nimeona nitumie hii mpya kabisa na wakati kuna malumbano ya wazee kuoa watoto wadogo.

Tatizo lenu mnafikiria kuwapeleka puta kuwachosha ndiyo wanaburudika matokeo yake mnawakera, jamani taratibu yenye mchanganyiko wa kila kitu inapendeza zaidi ukizingatia wanaume wa makamu haya wanakuwa wamestaafu wanachotaka ni burudani iliyotimia wala siyo machejo hovyo hovyo, kwa sababu wameona mengi na kupitia mengi kwenye uwanja huo wa faragha.

Mume wangu kanishinda

Mume wangu anauza nyama, kiufupi ndiyo kazi niliyompendea.

Lakini yatokanayo na kazi hiyo ndiyo yananichukiza, mume wangu haoni shida kuvaa nguo yenye madoa ya nyama ukimuuliza anasema hawezi kuyakwepa kwa sababu ndiyo kazi yake, hachani nywele bwana huyu, hapaki mafuta ukifanya masihara haogi siku nzima.

Nifanyeje?

Kwanza kosa ni lako yeye hastahili lawama, kama unakubali nguo zenye madoa zikae ndani lazima atazivaa, hivyo hakikisha unafua nguo hadi zinaisha madoa iwe kwa mikono au kwa kutumia dawa hilo ni jukumu lako. Usafi wa mume ni jukumu la mke moja kwa moja, halina ubishi.

Hili la kutochana nywele na kuoga linahitaji mjadala kati yenu wawili, ili kazi iwe rahisi na uifanye kwa muda mrefu bila kuchoka fuatilia malezi yake na historia yake tangu mtoto, inawezekana alizoweshwa hivyo kwao. Ukigundua alizoweshwa ujue kibarua hicho ni cha muda mrefu na kinahitaji uvumilivu.

Unaweza kutumia uanamke wako kumaliza tabia hiyo kwamba akitaka mzungumze kikubwa awe ameoga tofauti na hapo kaa mbali naye kwa sababu huo si ugonjwa ni hali ya kujitakia.

Ukifanya hivyo mara kadhaa atajistukia na anaweza kupunguza kama si kuacha kabisa, kuhusu kutochanya nywele mueleze anavyokutia aibu kwa wenzako na jinsi anavyokukera, kemea kwa mbinu unazoona wewe zinafaa.

Habari Anti!

Naomba kwa hisani yako useme na hawa wanawake wanaojichubua. Mwenza wangu anajichubua hadi ninamuogopa, hana doa hata moja ila ameng’aa kama nyama imetoka nje yaani ngozi yake haionekani.

Nimemueleza nimechoka nifanyeje?

Hiyo kazi rahisi, kwa sababu mikorogo ina madhara kiafya, anza taratibu kila unachohisi kinamchubua ukikikuta kitupe, fanya hivyo kadri uwezavyo tena tupa mbali ambako hatakiona. Baada ya hatua hiyo mtagombana au atahamisha na kuvificha mbali.

Usiishie hapo kama unaweza waeleze wazazi wake au jamaa zake wenye dhamana naye, huku ukifafanua madhara ya kufanya hivyo ikiwamo kile kinachotangazwa kila mara na Mamlaka ya chakula na Dawa (TFDA).

Inaonekana hana elimu ya masuala hayo na ameyaingilia kwa pupa, hivyo unaweza kwenda naye kwa daktari ilia pate elimu kuhusu madhara ya matumizi ya kemikali za kubadili rangi ya mwili.

Akigoma kabisa kuacha hakufai kwa sababu anajitafutia maradhi yatakayokuja kuigharimu familia na kuna hatari akwaambukiza watoto tabia hiyo ya kujichubua, tafuta namna nyingine ikiwamo kumrudisha kwao akajifunze tabia nzuri.

Columnist: mwananchi.co.tz