Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

ANTI BETTIE: Kiwanda cha nywele kimehamia kichwani kwake, nimfanyeje?

50937 Pic+kiwandaa

Mon, 8 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Anti nimechoshwa na mke wangu. Napata taabu nikilala naye kutokana na nywele zake kunigusa kila ninapomgeukia. Nalazimika kulala nimetizama upande mmoja, kukwepa nywele alizozijaza kichwani.Kuna wakati huwa nahisi anataka kuanzisha kiwanda cha nywele kichwani mwake.

Nifanyeje kukabiliana na hili?

Hakuna namna zaidi ya kumueleza mkeo kuhusu hizo nywele, inawezekana anajipamba kwa ajili yako akidhani unazipenda.

Onyesha kuzichukia ikiwezekana siku moja hamia ulale upande mwingine, akikuuliza mwambie umechoshwa na kiwanda alichoweka kichwani.

Akiona unamwambia kwa kumaanisha naamini ataacha tabia yake hiyo au atakuwa anaweka za wastani.

Zingatia hili: Wahenga walisema “Samaki Mkunje Angakia Mbichi Akishakauka Hakunjiki” huu usemi una maana nyingi, lakini mojawapo ni kama jambo hulipendi likemee mapema.

Nikimpiga tukio anaumwa tumbo

Anti nisaidie kwa hili, mke wangu kila nikimpiga tukio anaumwa tumbo.

Kadhia hii imekuwa ikisababisha tunakaa hadi mwezi mmoja hatujafanya hivyo nahisi nitapata kishawishi.

Nifanyeje?

Usiniambie mambo ya kishawishi unapooa unapaswa ukubaliane na kila hali ya mkeo. Unakaa mwezi unalalamika namna hiyo, akipata mtihani ukashauriwa ukae mwaka bila kumgusa si utakuwa na vimada kila kona.

Vunja ukimya sema naye

Nimekaa naye kwa miaka mitano, nimemuonyesha kila kitu kuwa nahitaji niwe wake, lakini sioni dalili ya kunifikiria.

Nashindwa kumueleza moja kwa moja kwa sababu tulikutana mahali ambapo kila mmoja anaamini mwenzake ni muumini wa kweli, hivyo nikimuanza nahisi atanichukulia tofauti.

Anti nifanyeje?

Acha kufanya vitu bila kufuata utaratibu. Kama kweli unampenda umewezaje kukaa naye miaka mitano bila kufanya jitihada zozote za kuhakikisha mnakuwa pamoja.

Umesema unashindwa kumwambia kwa sababu nyinyi ni waumini , ila sidhani kama utamtamkia unataka kumuoa atakataa.

Napata wasiwasi na nia yako, inawezekana una mipango tofauti, huwezi kukaa miaka mitano unamsubiri mwanamke na hujamwambia azma yako, ina maana kuna mahali unaburudika kwa maana ya kumaliza matamanio yako. Nakusisitizia fanya jambo moja muhimu nenda kwao kampose kwa nia ya kumuoa na si vinginevyo.



Columnist: mwananchi.co.tz