Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zuchu: Tunataka afande aliyewatuma wabakaji akamatwe

Zuchu Msgz Zuchu: Tunataka afande aliyewatuma wabakaji akamatwe

Tue, 20 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa muziki wa Bongo Fleva, Zuchu ameendelea kupaza sauti kutaka haki itendeke juu ya Binti wa Dovya aliyefanyiwa ukatili kwa Kubakwa na kuhimiza juu ya kukamatwa kwa afande ambaye anadaiwa kuwatuma wahalifu waliotekeleza ukatili huo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Zuchu ameandika kuwa; "TUNAMTAKA AFANDE ALIETUMA KUFANYIWA UNYAYASAJI BINTI YULE NAYE AKAMATWE.VIDEO ILE ILIJIELEZA WALA HAKUNA CHA KUFICHA KUWA KILE KIKUNDI KILITUMWA NA BOSS WAO ALIETAMBULIKA KAMA AFANDE MPAKA SASA HAKUNA JINA WALA SURA MUNAMFICHA WA NINI? KWAMBA YEYE ANA HAKI SANA KULIKO WENZAKE? KWA NINI HATUJUI HATA JINA LAKE? HATUTOWAELEWA KABISA @polisi.tanzania TUMTAKA NA AFANDE.

MUNAUMIZA HISIA ZA WATU HILI JAMBO LIKO WAZI SANA. NASIMAMA NA BINTI HAKI ITENDEKE @polisi.tanzania."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live