Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zuchu: Nimekumiss Diamond, RudiBasi

DIAMOND ZUCHU TENA.png Zuchu: Nimekumiss Diamond, RudiBasi

Wed, 27 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Malkia mpya wa muziki wa Bongo Fleva, kutoka WCB, Zuchu amekuwa na tetesi za miezi kadhaa sasa kwamba anatoka kimapenzi na bosi wake, Diamond Platnumz.

Sasa, taarifa ikufikie kwamba, mrembo huyo ameshindwa kuficha hisia zake kwa Diamond au Mondi wakati huu ambapo jamaa huyo yupo nchini Uingereza na barani Ulaya kwa ajili ya kutangaza albam yake fupi (EP) ya FOA.

Zuchu amefanya mazungumzo ya moja kwa moja (kwenda live) kupitia Mtandao wa Snapchat na Diamond akiwa kitandani nchini Uingereza, naye akiwa kitandani Bongo na kumueleza namna ambavyo amemmisi huku akiomba arudi nchini huku akitaka kutokwa machozi.

Diamond na Zuchu wamekuwa wakitrendi kwa miezi mitatu sasa ambapo wakiwa pamoja nchini huwa hawapoi kwani habari zaao huwa ni nyingi mno.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: