Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zuchu, Diamond wawavaa TCRA, BASATA "Uoga huzaa unafiki, mwisho umauti"

DIAMOND HDJSK Zuchu na Diamond

Sat, 7 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) pamoja na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)

Kuagiza kusitishwa kwa video ya wimbo wa Diamond Platnumz ft. Zuchu "mtasubiri" kutokana na kipande kinachoonesha Zuchu akiwa Kanisani kwenye kwaya kisha kuacha kuimba na kupokea simu masanii Zucu amewaandika barau ya wazi kupitia ukurusa wake wa Instagram.

Ni matumanini yangu mpaka sasa kila mtu anafahamu kua Video Ya wimbo wetu pendwa “MTASUBIRI “ Umesitishwa kuonekana kwenye vyombo vya habari Nchini kwetu .Nimeona bora nianze moja kwa moja kwenye mada husika.

Jana Nilipokea taarifa hizi kupitia mitandao kama Nyinyi tu mashabiki zetu kwamba wimbo wetu unapigwa marufuku sababu tajwa kua inaleta ukakasi kwenye jamii husika mwisho wa kununukuu .

Awali ya yote niseme kama msanii nilietumia ubunifu kukaa chini na muongozaji wa video yetu takribani siku 4 kuunda stori ambayo kwa utashi wangu na heshima niliyonayo kwa dini zote na madhehebu yake sikuona huu ukakasi unaoongelewa hapa.

Nafahamu si kila kazi ya kisanaa itamfurahisha kila mtu lakini kuvunjia heshima dini si kitu ambacho kipo ndani ya weledi wa kazi yetu sababu tunafahamu fika tunao mashabiki wa dini zote na kulinda hisia zao ni moja ya nguzo kuu Kwenye mziki hatueki matabaka .

Ifahamike kwamba mimi ndie nilishoot hiyo scene ikinataka kuwepo kanisani nikiwa nafanya mazoezi ya kwaya sio misa ni mazoezi ya kikwaya nikiwa nimevalia joho lenye stara .

Kanisa hili lipo kisarawe na kabla ya kushoot masister walitukagua na kusikiliza kwa makini stori yetu na kuridhishwa nayo ndipo hapo tukapewa ruhusa ya kushoot.

Naomba nielekeze malalamiko yangu kwa mamlaka husika BASATA walezi na wazazi nimeambatanisha video na movie baadhi ambazo zimetoka kabla ya mtasubiri vipi hizi hazina ukakasi .Lakini ni jamii ipi hiyo iliyoleta malalamiko mpaka nyie kufungia video iliyogharimu muda wa siku nne na pesa nyingi kuishoot tena mkaifungia bila hata kutaka kusikiliza utetezi .

Mtasubiri video ni ya kawaida sana A very innocent sweet story. HAYATI baba wa taifa alisema “Utii ukizidi huzaa uoga, Uoga huzaa unafiki na kujipendekeza mwisho wake Umauti“

Huu ndio umauti wa Tasnia hii unapoanzia .Sijui nileleze vipi hisia zangu zipokelewe kwa heshima ya kutosha na utii bila ya kuchukuliwa kama mjeuri ila kwa hili mumetuonea.

Sisi ni vijana tunaotafuta rizki bila ya kuchoka lakini pengine Wazazi wetu @basata.tanzania mmekua mstari wa mbele kutuvunja nguvu mbele ya jamii bila kujali hisia muda vipaji na uwekezaji unaofanyika .Hapo awali mlitoa mirabaha Wasanii wa Wcb Hatukunusa Top List Wakati kitwakwimu za namba.

MAUZO na ufanyaji vizuri Katika Chati zote Kasoro yenu nyinyi @basata.tanzania @cosotatanzania Nini shida wazazi wetu .Inawezekana vipi . Kisha hapo Tunalaumiwa kwa kutoshiriki Tuzo.

Ni wazi kua Hii imekua wazi sasa kama mamlaka ya kisanaa inafanya kazi Kupinga juhudi za WCB lakini pengine hii hasira mnayoipandikiza juu yetu tunaihitaji kwa mafanikio chanya yetu na mashabiki zetu wanaotupigania.

Mwisho niseme kazi iendelee Mashabiki zetu, Maboss zetu mtusamahe sana kwa kero mnayokutana nayo haiko mikononi mwetu Wenye mamlaka washasema sisi ni nani? Tuwe na subra na msituache mana nyinyi ndo kimbilio letu la mwisho Nawapenda sana. Sikukuu njema KAZI IENDELEE...

Diamond naye aka-comment chini yake

Najiuliza kuna baya lolote limefanyika kwenye hio scene? Mlivaa vimini? hapana!… Nlitwerk ama Mliimba matusi humo kanisani? Hapana! Mlivuta sigara au bangi humo? Hapana!… Mlikiss ama Kunywa Pombe humo Hapana!… Simu iliita, ulipokelea ndani? Hapana…je kushoot kanisani ni sisi wa kwanza?

Hapana! Kuna wengine walishoot Videos na Movie tena wao walifanya kwa kulidhalilisha kabisa kanisa… Nyimbo zao zilifungiwa??? hapana!

Halaf kesho utaniuliza kwanini Nilikataa kushiriki Tuzo za Basata… NCHI ya Wenyewe hii Zuuh… Kikubwa Mungu na Mashabiki wanatupenda hio inatosha… Tuendelee kuwawakilishia Taifa lao, leo bendera inapeperukia Ethiopia InshaAllah.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: