Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zari ammwagia sifa Zuchu "Ni msichana mzuri"

Zuchuuuu Zarii Zari ammwagia sifa Zuchu

Fri, 22 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mama watoto wa Mwimbaji Diamond Platnumz, Zarina Hassan (Zari The Boss Lady) ambaye amewasili Tanzania usiku wa kuamkia Machi 21, 2024 amefunguka kuhusu ukaribu wake na msanii Zuchu ambaye anatoka kimapenzi na Mondi, amesema ni Mtu mzuri na hata watoto wake wakiwa Tanzania huwa kwenye mikono salama na huwa anawasiliana na Zuchu kujua maendeleo yao.

Zari amesema; “Watu wanachukulia kwamba mimi siongeagi na wanawake wa Diamond, mimi naonega na mama Naseeb Jr (Tanasha), naongea na Zuchu hata kama watoto wanakuja Tanzania simtafuta hata Baba T (Diamond) kumuuliza mnaendelea huko, mko poa.

“Mimi huwa nampigia Zuchu moja kwa moja namwambia za asubuhi, mnaendeleaje huko, anasema tunaenda party au tunaenda kuogelea. Ni kwa sababu sioni tatizo kwake, kwanza ni msichana mzuri sana, na watoto wangu wakiwa huku wanakuwa na amani kuwa na yeye.

“Muda mwingi huwa nasema mbona umefanya hivyo? Ni kitu sahihi kwa mimi kufanya, nisipoongea na Zuchu wakati yupo na watoto wangu Tanzania, haileti maana,” amesema Zari.

Itakumbukwa hivi karibuni Diamond na Zuchu walikwenda Afrika Kusini na kukutana na Zari na mumewe Shakhib lakini siku chache baadaye kuliibuka mtifuano baada ya Diamond kupost video akitembea na Zari jambo ambalo lilizua mtafaruku baina yake na mpenzi wake Zuchu lakini baadaye mambo yalikwenda vizuri na wakaelewana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: