Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zari adai mtoto wa Diamond mtukutu

Diamond Tiffah Zari adai mtoto wa Diamond mtukutu

Fri, 22 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zari The Boss Lady; ni mwanamama wa Uganda penye pesa zake aliyezaa watoto wawili na staa wa muziki nchini Tanzania, Diamond Platnumz.

Zari na Diamond walikwa wapenzi kati ya mwaka 2014 hadi 2018 ambapo walibarikiwa na watoto wawili, binti Tiffah Dangote na na mvulana Prince Nillan.

Tiffah Dangote amezaliwa mwaka 2015 huku Prince Nillan akizaliwa mwaka mmoja baadaye. Licha ya kutengana kwao, Diamond na Zari bado ni marafiki wakubwa na wanaendelea kushirikiana katika malezi ya watoto wao.

Kupitia Instagram, Zari ameonesha jinsi mtoto wake wa pili na Diamond, Prince Nillan alivyokua mkubwa na jinsi ambavyo ni mtanashati na mchangamfu.

Zari ameposti picha za Nillan akiwa amevalia mkufu wenye maandishi ‘WCB’ ambayo kirefu chake Wasafi Classic Baby; lebo ya muziki inayomilikiwa na Diamond kisha akaandika; “Kwa nini anaonekana mzuri, lakini mtukutu…”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: