Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zamaradi aomboleza kifo cha paka wake

Zamaradimketema 1707480064510.jpeg Zamaradi aomboleza kifo cha paka wake

Tue, 3 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa uchungu mzito Mtangazaji, Zamaradi Mketema aomboleza kifo cha ghafla cha paka wake baada ya kushambuliwa na mbwa.

"Sijawahi kutegemea kama nitaumia hivi kwa kiumbe tofauti na mwanadamu, Paka wangu anaitwa HANNA, usiku sijui kitu gani kimemtuma atoke nje, kametokea dirishani akakutana na mbwa maana mbwa huwa tunawafungulia usiku tu wakamuumiza mno, na hii ni mara ya pili.

Mara ya kwanza alitokaga mbwa wakamshambulia bahati nzuri tuliwawahi akawa hoi lakini akapona kabisa akawa sawa, na akawa muoga kutoka ndani usiku sasa sijui kajisahau nini jamani katoka tena kilichomkuta this time hajapona, nimeumiaaaaa Mwan Kalikuwa karafiki kazuri sana, nikirudi tu nyumbani lazima anikimbilie, na kila ninapoenda anakuwa nyuma!!

"Na utakapokaa lazima kawe pembeni, na kuna muda kachokozi kwelikweli lakini ni usumbufu wenye raha ndani yake, Dah!! Nimeumia kwakweli," ameandika Zamaradi Mketema katika ukurasa wake wa Instagram.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live