Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

YouTube ya Diamond yarejea, wadukuzi wapita nayo tena!

Diamond Nikifa Diamond Platnumz

Tue, 26 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hatimaye YouTube channel ya supastaa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz imerejea tena hewani katika mtandao huo baada ya kuondolewa kwa saa kadhaa.

Channel hiyo ambayo ina siku mbili tangu idukuliwe (hacked), mapema jana ilikuwa imeondolewa na YouTube (terminated) kufuatia kukiuka masharti na kuvunja sheria zilizowekwa na kampuni hiyo huku video zote kwenye akaunti hiyo zikiwa hazipnekana.

Lakini, baada ya kurejea hewani, video za nyimbo za Diamond zinaonekana vizuri lakini bado jina linaonekana ni ARK Investiment badala ya Diamond Platnumz huku ikionyesha Live iliyoandikwa kwa kichwa cha habari "Elon Musk interview! Bitcoin & Ethereum Crash this month - ARK Invest"



Jambo hili linaonyesha bado YouTube account hiyo ina changamoto na huenda wadukuzi bado wanaishikilia.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Digital katika kampuni ya WCB, Kim Kayndo mapema jana alifunguka sababu za youtube kuiondoa channel hiyo, ambapo alisema;

"Kutokana na live iliyoruka siku ya Jumapili pindi channel hiyo ilipokuwa imehakiwa na kutoa maudhui yaliyovunja sheria za Youtube" alieleza @kimkayndo kupitia ukurasa wake wa twitter.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: