Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Will Smith amchapa Kibao Chriss Rock Hafla ya Tuzo za Oscar (+Video)

Video Archive
Mon, 28 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muigizaji kutoka nchini Marekani Will Smith, ametawala kwenye vichwa vya habari duniani asubuhi hii baada ya kumchapa kibao mchekeshaji Chris Rock live Jukwaani wakati wa ugawaji wa Tuzo za Oscars.

Chris Rock alifanya utani juu ya mke wa Will Smith, Jada Pinkett ndipo Will Smith aliamka na kupanda Jukwaani kisha kumchapa kofi la nguvu na kumwambia mara mbili “Keep my wife’s name out of your f-cking mouth“(Usiliweke jina la mke wangu ndani ya mdomo wako).

Chriss Rock aliongea utani kuhusu staili ya nywele ya Jada ambaye siku za hivi karibuni alizungumza kuhusu ugonjwa unaomfanya apoteze nywele zake, ambapo uzalendo ulimshinda Will Smith na kumfanya kwenda kumpiga kibao ChrisRock.

Baadaye WillSmith alipanda Jukwaani baada ya kushinda Tuzo ya Best Actor, kwenye hotuba yake alisema alifanya kitendo hicho kwa lengo la kulinda familia yake dhidi ya chochote.

Hata hivyo aliishia kuomba radhi mbele ya wahudhuriaji na kila mmoja aliyekuwa akitazama kupitia televisheni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live