Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vanessa Mdee avuta ndinga la Mil. 400 - VIDEO

Video Archive
Tue, 6 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenye nacho siku zote anaongezewa! Mrembo ambaye aliwahi kutamba katika ulimwengu wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee, mbali na kuishi Marekani, bado anaishi Maisha ya kitajiri na mzazi mwenzake Rotimi.

Vanessa ambaye aliondoka nchini miaka kadhaa iliyopita na kuhamia mzima Marekani, amekuwa akionekana akila bata kwenye maeneo mbalimbali nchini humo kuonesha kwamba pesa si tatizo kwake.

Ukiachana na bata, ame-Share Video Katika Ukurasa Wake Wa Instagram akilionesha Gari Lake Jipya Aina Ya ‘Mercedes-Benz- G class’ Alilojizawadia Hivi Karibuni.

Kwenye video hiyo inasikika sauti ya Vanesa akieleza kuwa baada ya kupata dili jipya lililowaingizia mkwanja, ameamua kujizawadia gari hilo la thamani kama sehemu ya kujifurahisha.

Vanessa ameonekana akiwa na Rotimi pamoja na mtoto wao wa kike wakielekea kwenye yadi ya magari hayo na kulipanda baada ya kukamilisha malipo.

Gari Hizo Thamani Yake Zinatajwa Kuanzia Kiasi Cha dola laki moja na arobaini na tano had idola laki moja na sabini na tano ambazo ni ni sawa na Tsh Milioni 400 Hadi Kiasi Cha Tsh Milioni 470.

Anyway Vannesa anaishi Maisha yake kwa sasa muziki sio kivile anafanya pale anapojisikia lakini uhakika ni kwamba, bata anakula na mumewe huko Marekani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live