Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vaa gauni kuonekana nadhifu

Uwoya Mrembo Vaa gauni kuonekana nadhifu

Wed, 10 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Gauni ni vazi la heshima na pendwa linalovaliwa na mwanamke. Unapovaa linakufanya mwili kuwa huru.Vazi hili huvaliwa sehemu yoyote na kumfanya mtu kuonekana mstaarabu.

Kuna aina mbili za gauni refu na fupi leo tunazungumzia gauni refu la usiku unaloweza kufaa kwenye shughuli fulani.

Zamani mwanamke tulizoea kuona magauni marefu ya usiku yakivaliwa Zaidi na maharusi, viongozi kwenye shughuli maalumu lakini sasa hali imebadilika. Vazi hili pia huvaliwa siku muhimu za shughuli za ibada n ahata mahakamani.

Yapo magauni ya aina tofauti tofauti yanayotoka nje ya nchi yakiwa yameshonwa huko hapa nchini kwa kutumia kitambaa vya kawaida au hata vitenge.

Ukiendakama kwenye harusi nyingi za kidini wakristo na waislamu magauni marefu ndio mavazi pendwa kwa maharusi na waalikwa.

Nguo ndefu zenye mipasuo mbele hizo ndio zimepanda chati sanakwenye shughuli za mastaa wengi wa kike wanaopenda kuvaa na mipasuo ya kutosha.

Gauni refu huwa halimkatai mtu yoyote ukivaa unaonekana nadhifu na mwenye heshima pia linakufanya uwe ni mwenye kujiamini.

Haimkatai mtu anavaamwanamke yoyote sio mnenewala mwembamba mrefu hata mfupi akivaa anapendeza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live