Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Safari ya Diamond Kigoma, behewa la treni lilivyobadilishwa kuwa klabu

Video Archive
Mon, 30 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Hakuna linaloshindikana ukiamua. Ndivyo unavyoweza kusema unapoingia katika behewa liliandaliwa maalumu kama klabu kwa mashabiki na wasanii walioungana na Diamond kwenda mkoani Kigoma kuazimisha miaka kumi ya kufanya kazi za kisanii.

Behewa zima limetandikwa zulia jekundu, huku pembezoni mwake kukiwa kumewekwa mito mirefu ikiwa imevishwa foronya za vitenge vya rangi tofauti tofauti na kubadili kabisa mwonekano wa behewa.

Mwisho wa behewa hilo kumetengwa sehemu maalumu kwa ajili ya DJ ambaye atakuwa akiyaburudisha masikio ya wapenda burudani watakaojumuika na wenzao katika behewa hilo lililobadilika jina na kuwa klabu.

Mbali ya hilo, pembeni ya DJ kuna mahali ambapo watu wanapata vinywaji muda wote, tangu mwanzo wa safari hadi mwisho.

Imezoeleka juu ya behewa kuna sehemu pa kuweka mizigo, lakini katika klabu hii ndani ya treni, eneo hilo limefungwa spika kubwa na ndogo zitakazokuwa zinampa nguvu DJ ya kuendelea kuangusha muziki mmoja baada ya mwingine.

Ukiingia katika klabu hiyo unapokelewa na taa (Nightclub Lighting), ambazo zitakufanya uamini kuwa kweli upo klabu unasakata muziki.

Katika kuta za behewa hilo au klabu ndani ya treni, kumepachikwa picha mbalimbali zikiwa na maelezo na picha ya mkali wa wimbo ‘Baba Lao.”

Mapema baada ya kuanza safari saa 2:05 asubuhi leo Jumamosi Desemba 28, 2019 msanii Diamond Platnumz anayeongoza msafara huo kuelekea Kigoma alilazimika kuweka kambi ndani ya klabu hiyo kuanzia stesheni ya Kamata jijini Dar es Salaam hadi Ngerengere Morogoro.

Kutokana na hilo, hata kukaa na familia yake ambapo katika safari hiyo yupo Dada yake Esma, mpenzi wake  Tanasha Donna, dada yake Queendarleen  na mtoto wao Naseeb ilionekana kuwa taabu.

Jambo ambalo lilimlazimu Tanasha  kumfuata mpenzi wake  huyo wakati wa kunywa chai katika klabu hiyo na kukaa naye chini kupata kifungua kinywa hicho.

Endelea kufuatilia Mwananchi kupata kinachojiri kwenye safari hiyo

Chanzo: mwananchi.co.tz