Dodoma. Waziri wa Afya nchini Tanzania, Ummy Mwalimu amempongeza msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ruby kwa mjasiri wa kueleza ukatili aliofanyiwa na mwanaume.
Waziri Ummy ametoa kauli hiyo leo Jumanne Novemba 26, 2019 katika uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili dhidi ya wanawake uliofanyika mjini Dodoma.
"Nampongeza sana Ruby ni msichana wa kuigwa, amesimama na kueleza ukweli wake kuhusu kile alichokuwa akifanyiwa, ni mambo mabaya ambayo hayapaswi kuvumiliwa katika jamii, imeniumiza zaidi," amesema Ummy.
Amesema licha ya kutosikiliza upande uliolalamikiwa, amesifu ujasiri wa msanii huyo kueleza suala hilo hadharani.