Staa wa Bongo Fleva, Barnaba amekiri kuwa ni kweli alibadili dini kutoka kuwa Mkristo na sasa ni Muislamu lakini akasisitiza kwamba hajafanya hivyo kwa shinikizo la Mwanamke bali ni maamuzi yake binafsi.
Kwenye Exclusive Interview na #Amplifaya CloudsFM, Barnaba ambaye jina lake jipya kwa sasa ni Mohamed na tayari amemchumbia Mrembo aitwae Raya ambaye pia ni Muislamu amesema;
“Nilibadili dini kwa mapenzi yangu na sio kama Watu wanavyotafsiri na nilibadili muda mrefu kama miezi sita imepita ila Watu wamejua juzi tu.
“Mimi ni Bwana Mohamed na hakuna sababu yoyote ya kusema labda Ukristo haujaniridhisha au Uislam ndio, hapana, Christian kwangu sawa, Islamic kwangu sawa lakini kwa sasa mimi ni Muislamu,” amesema Barnaba.
Novemba 2022, Barnaba alimvalisha pete ya uchumba mpenzi wake wa muda mrefu anayefahamika kwa jina la Raya kutoka Tanga baada ya kukaa singo kwa miaka kadhaa tangu alipoachana na mkewe wa awali.
Jambo lililowashtua mashabiki wengi ni kwenye utambulisho huo Barnaba baada ya kutangaza kubadili dini na kufuata dini ya mwanamke ya Kiislamu ambapo kuanzi sasa Barnaba ni Muisilamu na atajulikana kwa jina la Mohammed ingawa yeye amesema atapenda zaidi aitwe (MO).
Penzi la Barnaba na Raya limekuwa na kashikashi kwa mda mrefu ambapo familia ya Raya ilikiwa haimkubali kabisa Barnaba huku kikwazo kikubwa kikidaiwa kuwa ni utofauti wa dini lakini baadaye waliyanaliza.