Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

TikTok yakabiliwa na madai mapya ya kukiuka faragha ya watoto

TikTok Yakabiliwa Na Madai Mapya Ya Kukiuka Faragha Ya Watoto TikTok yakabiliwa na madai mapya ya kukiuka faragha ya watoto

Wed, 19 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tume ya Biashara ya Marekani imepeleka malalamiko dhidi ya TikTok na kampuni mama ya Uchina ya ByteDance kuhusu ukiukaji unaowezekana wa faragha ya watoto kwa Wizara ya Sheria.

Tume hiyo inasema uchunguzi wake "umefichua sababu ya kuamini" kwamba makampuni "yanakiuka au yanakaribia kukiuka sheria".

Katika taarifa kwa BBC News, msemaji wa TikTok alisema wamesikitishwa na uamuzi huo.

Kesi hiyo haihusiani na sheria iliyopitishwa mapema mwaka huu ya kupiga marufuku TikTok nchini Marekani ikiwa ByteDance haitauza programu hiyo.

Tume ya Biashara ya Marekani pia ilisema huwa haitangazi kwamba imepeleka malalamiko kwa Wizara ya Sheria lakini katika hali hii ilihisi kufanya hivyo ni kwa manufaa ya umma.

Kujibu, msemaji wa TikTok alisema kampuni hiyo haikubaliani na madai hayo na kwamba "imekuwa ikifanya kazi na Tume ya Biashara ya Marekani kwa zaidi ya mwaka mmoja kushughulikia wasiwasi wake."

"Tumesikitishwa na shirika hilo kuanzisha kesi badala ya kuendelea kufanya kazi nasi kupata suluhisho la kuridhisha," waliongeza.

Tangazo la tume hiyo linaongeza shinikizo linalozidi kuongezeka la TikTok nchini Marekani.

Mnamo Aprili, Rais Joe Biden alitia saini kuwa sheria mswada ulioipa ByteDance muda unaozidi mwaka mmoja hivi kuuza programu au kupigwa marufuku nchini humo.

Hiyo ina maana kwamba tarehe ya mwisho huenda ikafika muda fulani mwaka wa 2025, baada ya mshindi wa uchaguzi wa urais wa 2024 kuchukua madaraka.

Sheria ilianzishwa ili kushughulikia wasiwasi kwamba TikTok inaweza kushirikisha data ya mtumiaji na mamlaka ya Uchina - madai ambayo kampuni imekanusha.

Mnamo mwezi Mei, TikTok iliwasilisha kesi kwa lengo la kuzuia sheria hiyo, ikisema kuwa ni "uingiliaji wa ajabu wa haki za uhuru wa kujieleza" wa kampuni hiyo na watumiaji wake milioni 170 wa Marekani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live