Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Thom Cruise agonga miaka 62

Thom Cruise Dzc Thom Cruise

Wed, 3 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwigizaji wa filamu kutoka Marekani aliyejizolea umaarufu mkubwa Duniani kupitia mfululizo wa filamu za Mission Impossibe na Top Gun, Mtaalamu Thomas Cruise Mapother maarufu kama Thom Cruise ametimiza miaka 62 tangu azaliwe mnamo Julai 3 1962.

Tom Cruise alianza kuigiza miaka ya 1980s, ni miongoni mwa Waigizaji na Watayarishaji wa filamu ambao wanaingiza pesa nyingi sana kupitia filamu zao na inakadiriwa kuwa na utajiri wa zaidi ya Dola Milioni 600.

Tom Cruise amewahi kuoa mara tatu na ndoa zote zikavunjika, mara ya kwanza alimuoa Mwigizaji Mimi Rogers mwaka 1987, wakaachana mwaka 1990. Akamuoa Mwigizaji Nicole Kidman mwaka 1990, wakaachana 2001 kisha akamuoa Mwigizaji Katie Holmes mwaka 2006, wakaachana mwaka 2012.

Tom Cruise ana watoto watatu; Isabella, Connor na Suri ambao amewapata kutoka kwa wake zake wawili Nicole na Katie.

Filamu gani ya Tom Cruise unaipenda zaidi?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live