Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzia: Msanii Zahara afariki Dunia, sumu yatajwa

Video Archive
Tue, 12 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tasnia ya Burudani nchini Afrika Kusini imepata pigo lingine kutokana na kifo cha Mwimbaji Bulelwa Mkutukana "Zahara" (35) ikiwa ni miezi michache tangu kutokea vifo vya wasanii wengine #AKA (Februari 10, 2023) na #CostaTitch (Machi 11, 2023).

Zahara amefariki akiwa Hospitalini Jijini Johannesburg alikokuwa akipatiwa matibabu kutokana na matatizo ya ini yaliyoanza kumsumbua wiki mbili zilizopita.

Zizi Kodwa, Waziri wa Michezo, Sanaa na Utamaduni, alichapisha kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X/Twiter ujumbe uliosomeka: “Nimehuzunishwa sana na kifo cha Zahara. Pole zangu za dhati kwa familia ya yake na tasnia ya muziki ya Afrika Kusini”

“Serikali imekuwa na familia kwa muda sasa. Zahara na gitaa lake alifanya mambo ya makubwa na ya kudumu katika muziki wa Afrika Kusini,” alisema Kodwa.

Aidha, baadhi ya Vyombo vya Habari vimeripoti tetesi kuwa siku chache kabla ya kifo cha #Zahara, Dada zake walichukua Kadi za Benki za Msanii huyo na kwenda 'Shopping' huku ndugu yao akipigania uhai wake Hospitali

Inadaiwa chanzo cha kifo chake ni multiple organ failure iliyo sababishwa na yeye kulishwa sumu na mmoja kati ya wanafamilia mara baada ya Zahara kutolewa mahari.

Kabla ya kifo chake leo, Mwimbaji huyo amekua akizushiwa kifo mtandaoni hivi karibuni hadi kulazimu familia yake kukanusha mara kwa mara na kutaka Watu wamuombee mema.

Enzi za Uhai wake Zahara aliwahi kuja Tanzania Oktoba 2018 ambapo alitoa burudani Jukwaa moja na Juliana Kanyomozi wa Uganda, na LadyJayDee katika Tamasha la Vocals Night liliondaliwa na Lady JayDee.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live