Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TID: Walinishusha wakampandisha Diamond

Diamond And TID 1 TID: Walinishusha wakampandisha Diamond

Fri, 15 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Khalid Mohamed anafahamika zaidi kama T.I.D (Top in Dar) amesema baada ya kuanza kudai maslahi yake, wadau wa muziki waliamua kumshusha kimuziki na kumpandisha Diamond Platnumz.

"So Diamond was me lakini wakasema wewe siunajifanya mjanja sasa tunamleta Diamond tukushushe wewe,” alisema TID.

Ikumbukwe kuwa, Diamond aliibuka mwaka 2009, lakini alianza kuwa staa mkubwa kuanzia mwaka 2013 baada ya kuachia ngoma yake ya 'Number One' ambayo alimshirikisha staa wa Nigeria, Davido.

Mpaka sasa Diamond ndiye msanii namba moja Afrika Mashariki akifanikiwa kufanya vizuri kwenye muziki na kusimamisha biashara zake ikiwemo Wasafi Media, lebo ya WCB na biashara nyingine nyingi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: