Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TANZIA: Baba wa Kanumba afariki

98371 Baba+kanumba+pic TANZIA: Baba wa Kanumba afariki

Mon, 9 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Saalam. Baba wa marehemu Steven Kanumba amefariki dunia leo Jumapili ya March 8,2020 akipata matibabu katika Hospitali ya rufaa mkoa wa shinyanga. Taarifa za kufariki kwake zimethibitishwa  na mtoto wake Mjanael Kanumba, alipozungumza leo Jumapili March 8, 2020 na Mwananchi. Mjanaeli amesema baba yake amefariki leo saa nne asubuhi akiwa Hospitali ya rufaa mkoa shinyanga alipokuwa anapatiwa matibabu.

Mzee Kanumba kwa muda mrefu alikuwa anasumbuliwa na tatizo la nyonga lililosambabishwa kushindwa kutembea kwa muda mrefu na uvimbe katika kibofu cha mkojo pamoja na shinikizo la damu. Amesema msiba upo nyumbani kwa baba huyo  Ngokolo mkoani Shinyanga na utaratibu wa ratiba za mazishi bado zinaelendea.

Chanzo: mwananchi.co.tz