Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sugu; The Supreme Commander of The Streets

Sugu 2 Pic Data Sugu; The Supreme Commander of The Streets

Tue, 9 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Fourth July (Julai 4), kila mwaka, Marekani husherehekea siku ya uhuru wao. Ni siku muhimu na kubwa kwa taifa hilo. Jimbo kwa jimbo, na balozi za nchi hiyo popote zilipo, hufanya sherehe kwa kulipua fataki. Huo ni utamaduni.

Jana, Julai 4, 2024, ilitimia miaka 248 tangu kutolewa kwa Azimio la Uhuru wa Marekani, Julai 4, 1776. Oysterbay, Dar es Salaam, nyumbani kwa Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Michael Battle, Sr, ilifanyika sherehe iliyoandaliwa vema.

Hotuba ndefu yenye mantiki kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Afrika Mashariki, January Makamba. Risala nzuri ya Kiswahili ya Balozi Battle, yenye simulizi ya undugu wa kihistoria wa Tanzania na Marekani. Ushairi wa Zuhura The African Lioness. Wageni mbalimbali wenye nyadhifa. Chakula, vinywaji na mafataki kama ilivyo utamaduni.

Nilikuwepo shereheni. Masikio yangu yalikuwa hai, Balozi Battle aliposema, Joseph Mbilinyi "Sugu" ni rafiki yake. Akamtambulisha kuwa ndiye "founding father wa Bongo Flava". Kisha, leo (Julai 5, 2024), kupitia mtandao wa LinkedIn, Balozi Battle akamtambulisha Sugu kama "the original leader of Bongo Flava".

Nilikuwa timamu, bendi ya askari wanamaji kutoka Jeshi la Marekani, ilipoitwa jukwaani pamoja na Sugu. Kabla ya kutekeleza kilichofanya waitwe jukwaani, Sugu akazungumza machache, akasema ku-perform na bendi ya jeshi la Marekani, alijisikia kama "commander-in-chief of the streets".

Nisingependa kujadili performance ya "Sugu" na "Kiburi", ambazo ndiyo nyimbo Sugu alizigonga live na bendi ya jeshi la Marekani. Actually, the show was commanding. Ungestaajabu mabalozi na diplomats mbalimbali walivyochenguka na kazi adhimu iliyofanywa na Sugu jukwaani.

Ninachopenda kujadili ni mstari "ni VIP kila kiwanja ninachokwenda", ambao Sugu aliimba kwenye wimbo "Moto Chini". Juzi hapa, Sugu ametoka kushinda uenyekiti wa Chadema Kanda ya Nyasa. Januari 26, 2024, Sugu alikutanisha mabalozi na diplomats zaidi ya 10, Alliance Francaise, Upanga, kwenye event ya Bongo Flava Honors.

Mei 31, 2022, kwenye ukumbi wa hema (marquee), Hoteli ya Serena, Dar es Salaam, Sugu alifanya The Dream Concert. Mgeni rasmi alikuwa Rais Samia Suluhu Hassan. Akaweka rekodi ya kuwa mwana-Hip Hop wa kwanza duniani kumtoa ikulu rais wa nchi yake, kwenda kwenye event ya Hip Hop.

Mabalozi, viongozi wa siasa na corporate community, walihudhuria The Dream Concert. Sugu alikuwa anasherehekea miaka ya 30 ya uwepo wake kwenye muziki wa Hip Hop na Bongo Flava.

Mwaka 2010, Sugu aliweka rekodi ya kuwa mwana-Hip Hop wa kwanza ulimwenguni kushinda kiti cha ubunge, alipochaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini.

Sasa, jana, Sugu alipokuwa ana-perform na bendi ya jeshi la Marekani, tena wanajeshi wakiwa kwenye sare, akili yangu ilikuwa mbali ikiwaza. Sugu yuleyule wa “Siku Yangu” na “Ni Mimi” mwaka 1994 na 1995, ndiye huyohuyo miaka 30 baadaye anavunja diplomatic concert, akiwa amezungukwa na heshima kubwa.

The same Sugu aliyekuwa akiandika historia kwa kila wimbo aliotoa, “Hali Halisi” mpaka “Deiwaka”, “Nipo Fresh” hadi “Mambo ya Fedha”, status imeendelea kuwa VIP kila aendako. Inakumbusha mistari yake kwenye Moto Chini “labda huku nilipo nifuateni, maana naona inaonekana nitachelewa kushuka chini.”

Sugu alisema alijiona ni commander-in-chief of the streets. Iwe alisema kwa utani au alimaanisha, ila cheo kinamtosha. Asingekuwa mbunge bila kuijua na kuiweza mitaa. Asingebaki VIP kwa miaka 30 bila kuwa na nguvu ya kuiamuru mitaa. Asingefikisha albamu 10 za Hip Hop bila kujenga bond na mitaa.

Sugu ana-run successful event ya Bongo Flava Honors. Angekuwa ameshafeli endapo angekuwa hajui lugha ya mtaa. Sugu ni businessman, anamiliki Hotel Desderia, Mbeya, anakouza maandazi na chai, vilevile anatoa huduma ya vyumba vya kulala. Angeshafulia kama asingejua jinsi ya kuendeshana na mitaa.

Kutoka albamu ya “Ni Mimi” hadi “Veto”, rekodi alizoweka na kila historia aliyoandika safarini, kutoka kijana nusu balehe hadi dingi wa 52 years old. Ukichambua kila angle, utakubali kuwa Sugu yupo kwenye kundi la watu ambao wanayoyafanya hayaandiki historia, uhusika wao ndiyo historia yenyewe.

Mwalimu Julius Nyerere, aliyoyafanya yalivuka level ya kuandika historia. Mwalimu Nyerere mwenyewe akawa ndiye historia. The like of Bakhresa, Reginald Mengi, Youssou N'Dour, Jay Z, Andry Rajoelina, Volodymyr Zelenskyy na wengine mfano wao. Wenyewe ni historia, halafu historia zao ndizo zinashepu historia za nchi.

Sugu ni history na asingefika level hiyo bila command ya mitaa. Ndiyo sababu it’s well kwa kila mpenzi wa Mungu kwa Sugu kuitwa The Supreme Commander of the Streets. Historia yake ya mtaa ina-shape historia ya nchi hasa eneo la sanaa, hustles za mtaa na athari zake.

Ndimi Luqman MALOTO

Chanzo: www.tanzaniaweb.live